HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

2 June 2009

WAREMBO MKOANI TANGA WATAMBA

WASHIRIKI wa shindano la Miss Tanga Vodacom 2009,wametamba kuwa wamepania kuonyesha maajabu katika onyesho lao litakalofanyika juni mwaka huu katika uwanja wa mkwakwani. Walitoa maneno hayo jana wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wakiwa kwenye mazoezi ya onyesho hilo yanayofanyika ukumbi wa Splended Jijini Tanga. Wakizungumza mbele ya wakufunzi wao warembo hao walimweleza mwandishi wa habari hizi kwa nykati tofauti kuwa wamepania kupata taji la Miss Tanzania 2009 ili kuandika historia ya Mkoa wa Tanga. Warembo walio kwenye kambi ya Miss Tanga 2009 ni Shumu Hamad,Quen Paul,Irene Mahatane,Alice Marcus,Glory Chuwa,Joyce Joseph na Latifa Justine. Wengine wanaojinoa katikakambi hiyo tayarai kwa shindano hilo ni Neema Mbuya,Monica John,Rachel Mlaki,LinaLucas,Salma Halid,Christina Michael,Ramla Hassan na Agnes Sambo. Warembo haoa jana walikuwa kwenye mazoezi makali chini ya wakufunzi,Nadia Ahmed,Amina Sadick na OliverMango. Kwa mujibu wa maelezo ya Mkurugezni wa Five Brothres Enterteinment,Nassor Makau ni kuwa maandalizi ya shindano hilo yapo kwenye hatua za mwisho na kwamba mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa Said Kalembo Shindano hilo litakalofanyika uwanja waMkwakwani,limedhamini wa na Mwanaspoti,Vodacom,Picha nambari Jkt 015 na Jkt 016 ni washiriki wa shindano la Miss Tanga vodacom 2009 wakiwa katika mazoezi makali

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers