13 September 2012

BFT YAUNDA KAMATI YA MASHINDANO

               
Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limeunda kamati ya mashindano kwa lengo la kuhakikisha mashindano ya taifa  yanafanyika kwa kiwango cha taifa. Kamati hiyo imeundwa kwa kuwajumuisha wataalamu wa ufundi kutoka  kamati za BFT,mabondia wa zamani na wataalam wa mipango na fedha kutoka katika taasisi na mashirika ambayo yamekuwa mtari wa mbele kusaidia kwa vitendo shughuri na matukio mbalimbali ya BFT na kupelekea kusaidia kufuzu kwa bondia Selemani Kidunda  kushiriki katika michezo ya Olimpiki iliyomalizika hivi karibuni London, Uingereza.
Wajumbe walioteuliwa kuunda kamati hiyo ya mashindano ni Andrew kweyeyana ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati,Willy Issangura,Juma Suleiman,Remy Ngabo na Mohamed kasilamatwi.
Wengine ni Said Omari,Antony Mwang’onda,Joel Magori,Charles Jilaba na Undule Mwampulo.
Jukumu walilopewa ni kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa kufuata taratibu zote za chama cha ngumi cha dunia AIBA na kuhakikisha fedha za kuendesha mashindano zina patikana.
Majukumu ya kamati hiyo yatamalizika baada ya kumalizika kwa mashindano hayo
                                                                 Makore Mashaga
                                                                        Katibu Mkuu (
BFT)

No comments:

Post a Comment