18 December 2012

ZFA YAILIMA BARUA TFF

  Uongozi wa chama cha Zanzibar ZFA Kupitia Rais wa ZFA Ibrahim makungu kimeshaliandikia Barua  shirikisho la soka la Tanzania TFF ili  kutekeleza adhabu za wachezaji tisa wa Zanzibar kufungiwa kwa mwaka kutokucheza soka nje na ndani ya Zanzibar na kupinga hoja ya kuwa ZFA haina ubavu wa kuwafungia wachezaji hao.
kwani ZFA imesema wao ni wanachama wa CECAFA na inauwezo kuwafungia wachezaji kwani kitendo hicho kimefanyika katika mashindano ya CECAFA na hivyo adhabu hiyo kuanza mara moja wachezaji hao wa Zanzibar Heroes waligawana fedha wakiongozwa na Nadi Haroub  fedha hizo walizipata Mara baada ya kuifunga Tanzania Bara katika mashindano hayo, kama tff itaafiki basi wachezaji hao  watafungiwa mwaka mzima .
ZFA imesema kuwa kitendo hicho cha wachezaji hao hakivumiliki  na wametoa adhabu hiyo ili  iwe fundisho kwa wachezaji wengine .

No comments:

Post a Comment