HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

16 May 2013

HII SIO TAARIFA NZURI KWA WANAOPENDA ARSENAL


Bacay Sagna of Arsenal 

Mlinzi wa kulia wa klabu ya Arsenal Bacary Sagna ameshindwa kukataa kuwa yu karibu karibu kurudi nyumbani kwao ufaransa huku akipigiwa upatu wa kujiunga  Paris Saint-Germain au  Monaco wakati wa kiangazi .
Kandarasi ya mchezaji huyo wa kimataifa wa ufaransa inakwisha msimu ujao japokuwa anatarajia kuongeza kandarasi ya mwaka mmoja zaidi , Kijana huyo mwenye miaka 30-anaoneka kuwa wazi kuwa anaweza kuondoka klabu hapo.
"Yeah najiskia raha kuona PSG inanihitaji ni klabu inayovutia wengi ," Alinukuliwa katika  Le 10 Sport.
"Binafsi sijawasiliana na  PSG Na sijui kama wameongea na wakala wangu au ni tetesi tu  .
"Pale Arsenal, Hasa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kila mtu ananieleza kuwa nitaondoka na kwenda  PSG,Lakini hizo ni fununu tu  ,sijui nini kitakwenda kutokea .
"Nina weza kuongeza kandarasi yangu hapa  London lakini naweza kuondoka pia mwishoni mwa msimu  .bado nina mwaka mmoja umesalia Tusubiri tuone .
"Kwa sasa natazama nini kitafuata klabuni kwangu na . Nafikili nahitaji kuonana wakurugenzi juu ya kuongeza kandarasi yangu lakini Monaco inaweza kuwa changamoto mpya siko karibu na PSG ,lakini ni  Monaco au Arsenal.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers