HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

18 May 2013

HUYU MWAKYEMBE ANACHEKESHA !!!


 

Francis Cheka amesema si kwamba anakwepa kukutana na Benson Mwakyembe wa Songea bali bondia huyo hana uwezo wa kupigana naye ulingoni.

  Cheka amesema si kweli kuwa amewapiga mabondia wa Dar Es Salaam tu katika maisha yake kwani Karama Nyilawila anatokea Mbeya na Mada Maugo ambaye pia amewahi kupata kipigo kutoka kwake ni wa mkoa wa Mara.

Cheka alikuwa akizungumzia madai ya Mwakyembe ya wiki iliyopita kuwa bondia huyo wa Morogoro amekuwa akikwepa kukutana naye huku akijitapa kuwapiga wachezaji wa Dar Es Salaam tu.

Cheka alisema pia tangu 2008 amewapiga mabondia wa nje ya nchi katika ardhi ya Tanzania bila kupoteza pambano.

"Nyilawila sio wa Dar, maskani yake ni Mbeya, Maugo anatoka Mara, labda Kaseba, Rashid Matumla, Hassani Matumla na Mtambo wa Gongo (Maneno Osward) ndio wa Dar," alisema.

"Ila mimi sikuwa napigana na bondia kimikoa... hii sio michuano ya ridhaa ni ngumi za kulipwa yeyote anayekuja hutambuliwa bondia wa uzito husika na sio eneo analotoka.

"Lazima wanipe heshima yangu kama mabondia bora Tanzania kwa sasa, kama hawamheshimu bingwa wao wanataka wampe nani heshima hiyo?

"Waangalie nimetetea taji la IBF Afrika mara ngapi na kushinda, wapigane wenyewe kwa wenyewe waache nihangaike anga la kimataifa nililete heshima kama alivyofanya Snake Man (Rashid Matumla),

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers