HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

17 May 2013

LIGI YA MABINGWA KUPUGUZA BAADHI YA MIKOA WIKIEND HII

 
Mechi za marudiano za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zinachezwa wikiendi hii katika viwanja kumi tofauti wakati mechi ya Flamingo ya Arusha na Machava FC ya Kilimanjaro yenyewe itachezwa Jumatatu (Mei 20 mwaka huu).

Uamuzi wa mechi hiyo kuchezwa Jumatatu ni kutokana na Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid kutumika kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kesho wakati Jumapili utatumika kwa shughuli nyingine za kijamii kwa mujibu wa wamiliki wa uwanja huo (CCM Mkoa wa Arusha).

Mechi nyingine zitachezwa keshokutwa (Jumapili) ambapo Abajalo watakuwa wenyeji wa Red Coast kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara utatumika kwa mechi kati ya wenyeji Coast United na Kariakoo ya Lindi.

African Sports ya Tanga itaoneshana kazi na Techfort ya Ifakara mkoani Morogoro katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani. Nayo Simiyu United ya Simiyu itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua, mjini Singida.

Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ndiyo utakaotumika kuzikutanisha timu za Polisi Jamii Bunda kutoka Mara na wenyeji UDC wakati Biharamulo FC ya Kagera na Polisi SC ya Geita zitaumana kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Milambo FC ya Tabora itakuwa mwenyeji wa Saigon FC ya Kigoma kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora huku Mbinga United ya Ruvuma ikiikaribisha Njombe Mji ya Njombe kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa utatumika kwa mechi kati ya wenyeji 841 KJ dhidi ya Kimondo SC kutoka Mbeya. Nazo Rukwa United na Katavi Warriors zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

Timu zitakazofuzu kucheza raundi ya pili zitacheza mechi zao za kwanza kati ya Mei 25 na 26 mwaka huu wakati mechi za marudiano ni kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.

UTARATIBU WA SAFARI MECHI YA TAIFA STARS v MOROCCO
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litasaidia upatikanaji wa visa kwa waandishi wa habari na Watanzania wengine wanaotaka kwenda Morocco kushuhudia mechi kati ya Taifa Stars na Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.

Kwa ambao wangependa kupata visa kupitia TFF wanatakiwa kuwasilisha pasipoti zao, ada ya visa ambayo ni dola 50 za Marekani pamoja na picha mbili zenye kivuli (background) ya rangi nyeupe kabla ya saa 6 kamili Mei 20 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers