HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 June 2013

Gor Mahia KUZIBA NAFASI YA TUSKER KAGAME CUP


Gor Mahia 24102012
Gor Mahia -
Timu ya soka ya  Gor Mahia ya kenya imekubali kuchukua nafasi ya mabingwa wa kenya  Tusker katika mashindano ya CECAFA Kagame Cup ambayo yanatarajia kufanyika wiki chache zijazo .
Katibu mkuu wa timu hiyo   George Bwana  aliuambia mtandao moja wa www.starAfrica.com kuwa timu yake ipo tayari kuchukua nafasi hiyo .
Tusker imejitioa  katika mashindano hayo, kwa kile kinachodaiwa kuwa kutokuwa na uhakika wa usalama . Wameandika Barua kwa shirikisho la soka la kenya  (FKF) ambayo kopi ya yake ilielekezwa kwa katibu mkuu wa  Cecafa ikisema hawako tayari kushiriki michuano hiyo kwasababu hakuna uhakika wa ulinzi .
Aidha kwa upande wa katibu mkuu wa , Cecafa  Nicholas Musonye ambaye anakaa  Kenya amesema kuwa  Tusker itashughurikiwa kisheria na kinidhamu na kupigwa faini kwa kujitoa katika mashindano .
Bwana,anaongeza kwa kusema kamati ya utendaji imekutana na kuamua kuwa watapeleka timu ya vijana katika kuikuza timu yao ..amesema mashindano hayo yatawasaidia kujua ntimu yao ya vijana imefika hatua gani .
“Tulifanya mkutano na viongozi wetu na kulizungumzia jambo hili na tumekubaliana kuwa klabu itakubali mwaliko wa  CECAFA kushiriki mashindano hayo .
Gor Mahia ilimaliza nyuma ya  Tusker Mwaka  2012 ikiwa na alama  59 baada ya kucheza mechi   30 .
Wakati huo huo,Dirisha la usajili linaendelea  ,na klabu  hiyo imewaachia   Ali Abondo na  Moses Otieno ili kuleta nafasi kwa wachezaji wapya .
Japokuwa ,makamu wa rais wa kwanza   Faiz Magak amekataa kuwa wameachia huru wachezaji hao Abondo bado ana kandarasi ya mwaka mmoja lakini amekubali kuwa wamemwacha   Otieno.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers