HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

7 July 2013

MASKINI MAMIA YA WACHEZAJI KUPOTEA !!!!!!

            
Wiki hii nilipita katika Kiwanja cha kumbukumbu ya Karume sehemu ambayo, kunafanyika mashindano ya kuinua vipaji vya soka kwa wanawake na wanaume chini ya miaka kumi na saba.

 Jambo ambalo dunia nzima huwa inafanya katika Uendeshaji  wa soka Duniani kwakweli ni Jambo zuri na la kufurahisha na linapendeza sana kuona vipaji:-  Nilijionea Mengi sana hata katika soka ya wanawake kwani sijawahi kwenda kiwanjani  kutazama Soka ya kina mama zaidi ya kuutazama Kwenye runinga .

Jambo kuu kuliko yote Je ? vijana hawa baada ya hapa watakwenda Wapi ? Nilisikia kuna mpango wa kuchagua timu ya taifa ya mashindano hayo lakini je hawa wengine watakwenda wapi ?
Swari ambalo limeniumiza sana kichwa kiasi cha kushindwa kupata majibu ya uhakika nilikuwa natazama mapigo ya penati hapo ndipo nilipochoka kwani nilikuwa natazama mambo ambayo siku ya tegemea kidogo:-  makipa walikuwa wakirudi kaseja haoni ndani wapigaji walipiga penati za uhakika sana lakini bado najiuliza watahifadhiwa vipi wakina dada hawa ?

Kwa yule ambaye hakuwepo  kiwanjani na ninamuhakikishia yangemtoka machozi lakini kitu kikubwa nina amini Kuwa fikili Magoso Mchezaji wa zamani wa klabu ya soka ya Simba na Reli ya Morogoro atakuwa anakubaliana na mimi kwani hata yeye alikuwa amehudhuria nilimwambia kitu kimoja kuwa wakati wenu fursa kama hizi hazikuwepo ndio maana wachezaji wengi wa zamani wamekuwa na maisha ambayo hayalingani na sifa walizo kuwa nazo pindi wawapo kiwanjani!
    Shida kubwa ya Tanzania imekuwa ni jinsi ya kuhifadhi vipaji hivi mpaka kuna wakati Mkurugenzi wa michezo akauliza swari ambalo yeye ndiye mwajibikaji kuwa wachezaji hawa baada ya hapa watakwenda wapi ?
Mara nyingi nchi yetu imekuwa hodari wa kuanzisha mambo tena kisoka lakini mwendelezo umekuwa hafifu au kufa kabisa ukitazama hata timu nyingi zilizokuwepo zamani hasa wakati wa awamu ya kwanza na  mwishoni na ya pili katikati na mwisho zimekufa kutoka na sera mbovu za kimichezo na mtazamo usiofaa na matokeo yake kumeundwa timu za bonanza baada ya timu zao kufa kutokana na mawazo finyu katika mfumo wa uendeshaji .

Leo hii baada ya kufuta michezo mashuleni na kufuta sheria ya kwenda JKT tumepata vizazi ambavyo havina Dira!  Mashalow wamekuwa wengi kiasi kwamba hata kutandika shuka tu kwenye kitandanda anacholala ni ngumu  ,michuano hii ya Airtel Rising star imenipa dira ya kuona kama kuna uwezekano wa kupata pahala kwanini wasipatiwe  scholarship za kwenda kusoma katika Academy Mbalimbali ulaya kwani wamecheza wengi lakini ninachokiona hapo mbele ni kwamba tutapoteza wachezaji hawa.

 Kwani ni wengi kiasi kwamba hatutaweza kuwahifadhi kwakuwa hakuna sehemu tuliyoindaa kwa wachezaji hawa !
 Jambo kuu la msingi hata ukitazama Bajeti ya wizara ya Habari utamaduni na michezo pesa inazotengewa hazifanani kabisa na mahitaji ya soka la au michezo kwa Tanzania .Nyakati nyingine unaweza kujiauliza utumie lugha ya aina gani kuuleza umma kuhusu 
Ajira hii ya Michezo, Nadiriki kusema simba na Yanga ndio klabu kuu zinazo haribu soka la Tanzania kwani mara kadhaa zimekuwa hazijishughurishi sana maandalizi ya kisoka hasa kwa vijana hukimbilia zaidi kununua wachezaji wa kigeni Na wakati mwingine huwagombania wachezaji hao .
Leo kuna miradi kama hii bado haitoshi tunahitaji Taasisi zenye uwezo wa kutengeneza wachezaji kisoka zaidi ili waweze kuonyesha uwezo wao kwani sio wote wanaotakiwa kufanya kazi maofisini lakini unaweza kuona kama hatutatilia mkazo swala la kuinua michezo ni Ndoto kushiriki michuano ya aina yoyote .

Jambo kubwa na la msingi kwa sasa na kwa watanzania ni kuhakikisha tunaanzisha Taasisi za kisoka kama hizi kwani hofu yangu kubwa ni kwamba vipaji tunaviona lakini tunaweza kuwapoteza vijana hawa kwani hakuna pakuwahifadhi Tunahitaji shule ya michezo.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers