HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

4 July 2013

VIONGOZI WA KIKAPU TANZANIA HUU NDIO WAKATI WA KUMTONGOZA JK !

 


 

Mwanzoni  mwa wiki hii Dunia ili imulika Tanzania baada ya  Rais wa taifa kubwa duniani Barack Obama wa Marekana  alipofanya ziara ya siku mbili nchini, kabla hawajaanza kuzungumza jambo lolote na waandishi habari katika viwanja vya Ikulu jijini Dar Es salaam Barack Obama alishindwa kujizuia na akaanza kwa kusema kuwa tumezungumza vitu vingi na Rais Kikwete lakini bahati mbaya tumesahau kuzungumzia swala Hasheem Thabit kwa!  wale wasiomjua huyu ni kijana anayecheza mpira wa kikapu kule nchini Marekani akiwa na timu ya Oklahoma City Thunder

Inawezekana ilimuuna kusahau jambo hilo lakini jambo pekee lakujivunia kwa wanaopenda mpira wa kikapu kwa sasa ni kwamba Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete naye ni mchezaji mzuri  wa mpira wa kikapu kwa hiyo Marais hawa wawili ni wachezaji wa mpira wa kikapu kwa hiyo huu ni wakati muafaka wa Viongozi wa Mchezo wa kikapu Tanzania Kumtongoza Rias wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama sio kujenga kiwanja kipya basi kuwaachia hata shule ya mchezo wa mpira wa kikapu ili vijana wetu wapate kuujua na kuufahamu mchezo huu kiundani zaidi .
Lakini hili sio jukumu la Kikwete ni la Viongozi wa Shirikisho la mpira kikapu Tanzania Kumuandikia Proposal Mh Rais ya nini wanataka kabla hajaondoka madaraka kwani kwa muda uliobaki ni Eidha ajenge mwenyewe au amuachie deni Kiongozi anayaefuata. Hili jambo la kheri kwa wapenzi wa kikapu kwani ni muda muafaka kutembelewa na Rais ambaye Nchi yake ndio inayoongoza duniani kwa mchezo wa mpira wa kikapu duniani  kuliko nchi nyingine yoyote kwakuwa kuna ubia unaendelea baina ya Tanzania na Marekani huu ndio  wakati wa TBF kumtongoza Jk ili awaachie shule au uwanja wa kikapu !

Hasheem Thabeet cropped.jpg
Endapo Atawaachia shule ya kikapu itakuwa Bora zaidi kwani kuna mambo mengi yatanikiwa katika mchezo huo kwanza itakuwa ipo chini ya Marekani kwa muda kama ulivyokuwa uwanja wa taifa kumilikiwa na wachina  pili itakuwa ni fursa kuletewa wakufunzi kutoka marekani kuja kunoa makocha na wachezaji na kutasaidia kupata mafunzo mengi zaidi kwa watanzania kuliko kuchukua wachache na kwenda nao marekani ,Tukijenga shule  ya kikapu kutasaidia zaidi  kupata wasomi wengi zaidi wa mchezo huo .

kwa sasa Tanzania inashindwa kung'ara katika kila mchezo kutokana na kukosa miundombinu ya kimichezo ambayo imeshindwa kuimalika kwa muda tena tangu Marehemu  Rais nyerere aondoke madaraka takriban miongo miwili iliyopita kwa sasa jambo kuu kuliko yote ni nafasi ya TBF waliyoipata katika kung'ara kwenye mchezo huo  hii ni  bahati Gani? Tena ya Mtende hasa wakati huu ambao Tanzania imeingia ubia na rais mwenye nguvu kubwa Duniani tena mweusi na mwenye asili ya Afrika Mashariki .

Enyi TBF mnatakiwa kuchangamkia dili hii kabla JK hajasahau kwani akisahau itakula kwenu kwani Mh Rias ana mambo mengi ya kufanya na yanayomnyika Usingizi kila kukicha sasa kama mtaendelea kung'ang'aa Macho wale wajaruo wana hasira kijana wao hajaenda Kogelo Tangu aukwae Urais hii ni kama Bahati ya Mtende kwenu nitawaashangaa sana kama mtaiacha Neema hiii ambayo imekuja kwenu ni kama kuokota dhahabu sehemu ambayo hakuna hata Mgodi wa dhahabu .      

TBF CHONDE FANYENI KWELI 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers