HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

16 January 2013

BONDIA IDDY MNYEKE AJIFUA KUMKABILI SADIKI MOMBA FEBRUARY 14

 
 Bondia Iddy Mnyeke kulia akioneshana umbwamba wa kutupiana masumbwi na Mussa Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala  Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam

BONDIA Iddy Mnyeke yupo katika maandalizi mazito ya kujiandaa na mpambano wake na Sadiki Momba utakaofanyika  February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam

Bondia huyo kwa sasa ananolewa na kocha wa kimataifa wa Mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo wameweka kambi ili kumkabili Momba
Akizungumza Super D alisema kuwa amemwingiza kambini bondia wake ili aweze kumtengeneza vizuri kwa ajili ya mpambano wake na Sadiki Momba

Super D alisema kuwa mpambano huo utakuwa wa utangulizi kabla ya Deo Njiku na Omary Ramadhani kutwangana kugombea Ubingwa wa Taifa wa PST 
Kocha huyo alisema kuwa kambi yao itahakikisha inaendeleza ubabe baada ya bondia tegemeo wa kambi hiyo Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kumdunda Saidi Mundi Kutoka Tanga
Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina.  michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema.
 Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.   
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

 

Khaira Arby KUTUMBUIZA SAUTI ZA BUSARA

Tamasha la Muziki la Sauti za Busara kwa mwaka huu litafanyika eneo la mji mkongwe Zanzibar, kuanzia tarehe 14 hadi 17 Februari, jitihada zimefanyika katika kufanikisha tamasha la 10 na kuhakikisha kuwepo kwa uhuru wa kujieleza kupitia nyimbo mbalimbali  za wasanii wa Kiafrika ambao nyimbo zao zimepigwa marufuku au kuzuiwa katika nchi wanazotoka.
 
Kutakuwa na waimbaji wengi mahiri, akiwemo muimbaji  mwenye misimamo kutoka jamii ya kiisilam nchini Mali, anaejulikana kwa jina la Khaira Arby ambae alifungiwa kuimba licha ya kwamba nyimbo zake zinamsifu/ elezea Mtume Mohammad (SAW). Mwengine ni Comrade Fasto anayetoka Zimbabwe, msanii mahiri wa kurap na mshauri, ambae nyimbo zake zinakosea serikali ya Mugabe hali iliyopelekea nyimbo zake kutopigwa katika radio na Televishen ya taifa. “Tuna uwezo wa kufikisha ujumbe wetu kwa walengwa. Tuna timu  nzuri( mitaani) zenye uwezo wa kusambaza kopi nyingi za albam katika maeneo mbalimbali na hata katika mabasi ya abiria ambayo mengi yanatumiwa na wazimbabwe wa kawaida. Tumebuni njia mbadala “Radio Watu” na albam imekuwa zikichezwa katika vyombo mbalimbali vya usafiri”. Alisema Comrade Fasto.  
 
Wakati wa kongamano lijulikanalo kama Movers & Shakers ya Sauti za Busara, jopo la wasanii litafanya majadiliano ya kuangalia umuhimu wa kulinda uhuru wa kujieleza kwa wasanii. Nae Rebecca Corey, Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions anaamini kwamba ni muhimu kwa wasanii kupata nafasi ya kupaza  sauti zao. “Muziki ni njia moja yenye nguvu, lazima tuseme hali ya kutokuwa na usawa, tufurahie maisha, na kueleza hali ya utu wa mtu. Uhuru wa kujieleza ni haki za binadamu, na unatunufaisha sote ikiangaliwa na kuheshimiwa. Ndio maana Sauti za Busara ina jivunia kukuza sauti za wasanii kama Khaira Arby na Comrade Fasto ambao wamepigwa marufuku katika nchi wanazotoka”.
 
Msanii Khaira Arby kutoka Mali atafanya onesho lake katika tamasha la 10 la Sauti za Busara siku ya mwisho ya tamasha litakaloanza tarehe 14 hadi 17 Februari pale Ngome Kongwe, Zanzibar. Akivutiwa na binamu yake  Ali Farka Toure, Khaira Arby katika muziki wake ameweka vionjo vya chimbuko la  Berber na Songhai ambapo umekuwa ukileta mchanganyiko mzuri wa kuvutia wa desert blues na  wakati wa kurikodi huchanganya na kinanda cha guitar la umeme, ngoni, ngoma na muziki wa kitamaduni na kuufanya mziki wake uvutie sana. Arby, amezaliwa katika kijiji ambacho hakipo mbali na mji wa Timbutku, ambao umezungukwa na jangwa.
 
Kwa upande mwingine,  Samm Farai Monro, anaejulikana zaidi kama  Comrade Fatso, ni mmoja wa msanii ambae ni maarufu na anavuma kwa mashairi Zimbabwe.  Anaimba mashairi ya Toyi Toyi, mashairi ya mtaani yenye msimamo ambayo anachanganya na lugha ya Shona na kiingereza na mbira pamoja na hip hop. Atafanya onyesho lake sambamba na kundi la Tanzania Mlimani Park Orchestra wajulikanao pia kama Sikinde, Atongo Zimba kutoka Ghana, N'Faly Kouyaté kutoka Guinea, Owiny Sigoma Band kutoka Kenya, pamoja na wazimbabwe wenzake Mokoomba.
 
Miongoni mwa wasanii kutoka Tanzania watakao shiriki katika tamasha la mwaka huu ni pamoja na  Msafiri Zawose na Sauti Band, Lumumba Theatre Group, Super Maya Baikoko, Peter Msechu na wengineo wengi..
 
Kiingilio kwa watanzania ni shilingi 3,000 na kiingilio maalumu kwa wakaazi wa Africa Mashariki.
 
Kwa maelezo zaidi na picha downloads:  Tafadhali tembelea wovuti ya www.busaramusic.org                                                                                  

Pep Guardiola:KUANZA KAZI MSIMU UJAO Bayern Munich

Pep Guardiola

Klabu ya Ujerumani ya  Bayern Munich imetangaza kuwa Mkufunzi wa zamani wa Barcelona  Pep Guardiola ataichukua timu hiyo mwishoni mwa msimu  

Kijana huyo mwenye  miaka 41 alikuwa akihusishwa na kujiunga na  Chelsea na Manchester City - amatia saini kandarasi ya miaka mitatu mpaka  2016.
Guardiola atakuwa anaziba nafasi ya   Jupp Heynckes,ambaye anastafu mwishoni mwa msimu 
 
Bayern kwa sasa wako juu kwa Alama tisa zaidi wakiongoza ligi na wanatarajia kukutana na Arsenal mwezi ujao katika hatua ya kumi na sita bora ya ligi ya mabingwa .

Heynckes, 67, aliimbia klabu hiyo kabla ya  Christmas kuwa Hato ongeza kandarasi baada ya majira ya kiangazi .
Mkurugenzi mkuu wa Bayern'  Uli Hoeness Amesema kuwa : "Tunahijati Mkufunzi wa aina ya  Guardiola' ndiye anayeweza kuichukua nafasi ya  Jupp Heynckes."

Jocquis Sconiers AANZA KIBARUA LEO (TBF)

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjnhgAYsmfp1dOutqaDa42ZBhkIBgqNiOKPRzf1bBDm7Z1SMO8UAWuvBf_g-gLxtnv1nB85UN50586dt-uLtiET7gZA1akODvAkuvFIilMjB6U0Tpl11cHQcZ3lovLo31cLMCo48M_Hs1I/s1600/IMG00988-20121102-1956.jpg

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu, Jocquis Sconiers   anatarajiwa kuanza kazi ya kuinoa timu ya taifa ya wanawake na wanaume ya mchezo huo kwenye uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Sconiers ametua nchini huku akiwa na mikakati kadhaa aliyodai kuwa ikitekelezwa vyema, mchezo wa mpira wa kikapu nchini utsonga mbele kwa kiasi kikubwa na pengine  kuzipiku timu za mataifa ya jirani kama Kenya na Uganda.


Hata hivyo, kocha huyo amebakiwa na wiki moja tu kuinoa timu hiyo kabla ya kuanza kwa michuano ya mchezo huo ya Kanda ya Tano ya Afrika itakayofanyika jijini Dar es Salaam.

  Katibu msaidizi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Michael Maluwe, amesema wamefurahishwa na ujio wa kocha huyo na kuwataka wadau kumpa ushirikiano.

"Tunaomba wachezaji na wadau wa kikapu nchini wampe ushirikiano ili afanye kazi yake vizuri na kusaidia timu zetu," aliongeza  Maluwe.


Aliwataja baadhi ya wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho kuwa ni Ladislaus Ikungura,Gerald Baru, Abdallah Ramadhani ‘Dulla’, Henry Mwinuka ‘kidume’ na

Sudi Abdulrazak.

Wengine ni Sylivian Yunzu (Maige), Mussa Chacha, Frankline Simkoko,Small Forward, Mohamed Ally ‘Dibo’, Amir Muhidin Saleh na nahodha, Lusajo Samwel.


Kocha Bahati Mgunda alisema katika timu ya wanaume alikuwa na wachezaji 32 lakini sasa wamechujwa na kubaki 18 ambao watatu kati yao watapunguzwa zaidi na kubaki 15.

Pep Guardiola:NATAKWENDA UINGEREZA WAKATI HUU

 

 

Kocha wa zamani wa klabu soka ya Barcelona  Pep Guardiola amezungumza kwa mara ya kwanza kuwa anataka kupata changamoto mpya kwa kufundisha klabu moja wapo nchini uingereza .
Guardiola, ambaye ameipatia Barca mataji  14 katika misimu minne anaonekna kutafuta kibarua kipya kwa sasa . 
Pep 41 amesema kuwa akiwa kama mchezaji akufanya maamuzi ya kutaka kucheza soka uingereza lakini siku za usoni anatarajia kuwa mkufunzi katika soka la uingereza 
."
Kwa maneno haya Man city ,Chel,na united timu ambazo zinaamini kuwa zinahitaji hasa saini ya mkufunzi huyo na zimekuwa zikimfuatilia Guadiola zinaweza kufanikiwa kumpata  na hii inakuja mara baada ya Jose Mourinho kuonyesha dhahiri kuwa anataka kurejea uingereza 

Guardiola aliongeza kwa kusema : " Ni kitu cha kipekee kucheza ligi hii .Nataka kuona hisia za mashabiki, Mzingira , Vyombo vya Habari aina ya wachezaji  na kila kihusucho ligi ya Uingereza  
kiukweli ni ligi bora ukizingatia mimi bado mdogo .
" Guardiola Kwa sasa anaishi  New York na familia yake baada ya kuamua kuchukua mapumziko ya mwaka mmoja

Loic Remy NA  Yann M'Vila

 Yann M'Vila

Loic Remy




Kocha wa Queens Park Rangers  Harry Redknapp amesema kuwa  Loic Remy amefaulu vipimo vya afya na sasa kinachofanyika ni makubariano binfsi kati ya yeye na klabu husika na amesma yuko karibuni  kumtia kwapani kiungo wa ufaransa  Yann M'Vila.
Mshambuliaji wa Marseille Remy, 26,alionekana kwenda  Newcastle lakini sasa atajiunga na QPR kwa ada ya uhamisho wa pauni  £8m, wakati kiungo wa  Rennes  M'Vila, 22, anatarajiwa kuwagharimu pauni  £7m.
Redknapp amesema alivutiwa kusainisha wachezaji ambao anaona  wanaafaa kwa klabu yake 

"na ameongeza kuwa anatarajia kumnasa mshambuliaji wa West Brom Peter Odemwingie kwani tumesha pereka maombi ya kumsajiri lakini inaonekana imezimwa  na una haki ya kumuhitaji ni mchezaji mzuri kocha huyo bado anamsaka Mlinzi  Jonas Olsson na Kiungo wa Tottenham  Jake Livermore.
  QPR waliifunga   West Brom 1-0 na kuingia hatua ya nne ya michuano ya FA na kundelea na Takwimu  ya kutokufungwa mwaka   2013

YUSUPH MANJI AITAKA TFF BAADA YA KUICHUKUA YANGA




 Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangenzi ‘Zamunda’ akimchukulia fomu ya
 kugombea Uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu kwa niaba ya klabu za Ligi Kuu zilizompendekeza, Mwenyekiti wa Yanga SC, Yusuf Mehbub Manji (kulia) ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania 
(TFF), Ilala, Dar es Salaam mida hii, kuelekea uchaguzi utakaofanyika Februari 24, mwaka huu
 mjini Dar es Salaam. Anayetoa fomu hiyo kushoto ni Ofisa wa TFF, Jonathan Aloyce Kakwaya. 

Binzubery undstand

Jamal Emil Malinzi ,Nyamlani kuwania Urais TFF


 See full size image


 Wadau watatu wa mpira wa miguu wamechukua fomu za kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kufanya idadi ya waliojitosa katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 mwaka huu kufikia 30.

Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.

Waliochukua leo (Januari 16 mwaka huu) kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Jamal Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo.

Mwengine aliyechukua leo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuwakilisha Kanda ya Iringa na Mbeya.

Orodha kamili ya wadau waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais), Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (umakamu wa rais).

Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).

Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).

Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.

WAHARIRI, WAANDISHI WAPIGWA MSASA KANUNI ZA UCHAGUZI
Wahariri na Waandishi wa Habari zaidi ya 40 wameshiriki kwenye semina kuhusu Kanuni za Uchaguzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyofanyika leo (Januari 16 mwaka huu).

Wawezeshaji katika semina hiyo iliyofanyika ofisi za TFF walikuwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Deogratias Lyato na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah.

YANGA YAANZA MAZOEZI MCHANGANI



Timu ya Young Africans imeanza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Kijitonyama mabatini kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom na mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Black Leopard kutoka nchini Afrika Kusini siku ya jumamosi mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa jijiji Dar es salaam.

Young Africans ambayo imerejea siku ya jumatatu alfajiri ikitokea nchini Uturuki ambako ilikuwa imeweka kambi ya mafunzo kwa takribani wiki mbili, iliwapa wachezaji wake mapumziko ya siku mbili kabla ya leo tena wachezaji wote  kuanza mazoezi.

Wachezaji wote waliokuwa na timu katika kambi ya mafunzo nchini Uturuki wameanza mazoezi huku umati wa watu wengi ukijitokeza kuwaona vijana wa Jangwani ambao tangu warejee nchini leo ndio ilikua wanaanza mazoezi katika ardhi ya nyumbani.

Mchezo wa jumamosi dhidi ya timu ya Black Leopard utakua ni mchezo wa kwanza kwa Young Africans katika aridhi ya nyumbani katika mwaka mpya wa 2013 hivyo watatumia fursa hiyo kuwaonyesha washabiki ufundi walioupata kutokana na kambi hiyo ya mafunzo mjini Uturuki.

Timu ya Black Leopard inatajiwa kuwasili siku ya alhamis asubuhi ikitokea nchini Afrika Kusini tayari kabisa kupambana na mabingwa mara 23 wa ligi kuu ya Tanzania bara na mabingwa mara tano (5) wa kombe la Kagame.

Yanga itaendelea na mazoezi yake kesho asubuhi katika uwanja wa Mabatin Kijitonyama kujiandaa na mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mzuri wenye upinzani na wakuvutia ikizingatiwa timu ya Yanga ilikuwa kambi ya mafunzo nchini Uturuki ambao ilipata nafasi ya kuwa pamoja na mwalimu kuwafundisha wachezaji wake pamoja.
Viiingilio vya mchezo huo ni Tsh 30,000/= VIP A, Ths 20,000/= VIP B, Tsh 15,000/= VIP C , Tsh 7,000/= Orange na Tsh 5,000/= Blue & Green.

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers