HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

17 January 2013

aaAAAH SUAREZ VP WEWE ????

 


Mshambuliaji wa liverpool, Luis Suarez, ana amini kuwa analengwa sana na vyombo vya habari vya Uingereza lakini amekiri alijiangusha katika mechi moja ya ligi kuu msimu huu.
Katika mahojiana na kituo kimoja cha habari cha amerika ya kusini, mshambuliaji huyo kutoka Uruguay, amesema kila mara yeye hufwatilwa  pakubwa na mashirika hayo kwa kuwa jina lake huchangua  magazeti kuuza zaidi.
Suarez ambaye ndiye mfungaji bora wa liverpool msimu huu huku akiwa amefunga magoli 15, mawili nyuma ya nyota wa manchester United Robin van Persie, amekiri alijiangusha wakati wa mechi yao na Stoke City tarehe saba October mwaka uliopita.
Tangazo hilo la suarez limemuudhi kocha wa liverpool brendan roggers, ambaye amesema, mchezaji huyo ataadhibiwa kuambatana na sheria za klabu hiyo.
Roggers, ametaja tangazo hilo la Suarez, kama moja ambalo kamwe halikubaliki.

 
Suarez sasa amewagadhabisha makocha wa timu zingine zinazoshiriki katika ligi kuu ya Premier, na pia mashabiki ambao wanahisi kuwa mchezaji huyo hujiangusha bila sababu.
Mwaka uliopita, mlinda lango wa Swansea, Ashley Williams, alisema kuwa Suarez hujiangusha kuliko wachezaji wote ambao amewahi kucheza nao.
Mapema mwezi huu Suarez, alishutumiwa sana kuhusiana na jinsi alivyofunga bao la pili la Liverpool, baada ya kuunawa wazi mpira wakati wa mechi hiyo ya kuwania kombe la FA dhidi ya Mansfeild Town.
Lakini kocha wa Liverpool, alimtetea mchezaji huyo akisema kwamba aliunawa mpira bila kukusudia, lakini siku iliyofuatia, vyombo vya hjabari vya Uingereza vilichapisha habari yenye mada, Suarez ni mdanganyifu na mlaghai mkubwa.
Tangu alipojiunga na Liverpool mwaka wa 2011, mchezaji huyo ameandamwa na sakata nyingi.
Amepigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi nane, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha ya ubaguzi dhidi ya mchezaji wa Manchester United Patrice Evra na baada ya kumaliza adhabu hiyo, alikataa kumsalimia Evra katika mechi iliyofuatia, hatua iliyomkasirisha sana kocha wa Man United Sir Alex Ferguson.
 

WASANII KUUZA KAZI ZAO KIMATAIFA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh41XiAuplVdzQZ59c0_d86LFhZbHDvcG5M94PRBlcZ5plMSRzmfrsbZywnmGqyEQn9aH0c_43Gygu2v_wMzf6uNnxBJH3mYdSOEhttShr75kAO2HJG2bkMZ2ogfEtYLrbQPjR1EI2RnXih/s1600/DSC_8498.JPG 
Msanii wa filamu, Steve Nyerere (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.  

KAMPUNI ya Mad Mad Entertainment iliyopo jijini London nchini Uingereza, imeanzisha program maalum ya kupeleka wasanii wa filamu za bongo nje ya nchi kwa lengo la kukuza sanaa hiyo hapa nchini.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Yasmin Razak alisema ameamua kufanya kazi na wasanii  hao ili kuleta mabadiliko na kuwakwamua kiuchumi wasanii wa filamu hapa nchini.

 “Kwa muda mrefu niliokaa London sioni kama sanaa hii ina maendeleo, nikafikiria kitu gani nifanye ili  kukuza tasnia hii, katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza filamu na wasanii wa nje atalipwa kiasi cha sh 50 milioni pamoja na malipo mengine yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nchini.
“Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo na pia Ghana, Congo na hata Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema Tanzania nao kuingia katika mchakato huo,”alisema Razak.
Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa,  alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu,  kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.
Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.
“Hapa kuna kuinua vipaji, soko la kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu kwa wale watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo katika hatua za awali za mchujo,” alisema
Mwakifamba.

Naye muigizaji Issa Musa maarufu kama Cloud, alisema kuwa lugha itakuwa ni tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi, hivyo kuitaka kampuni hiyo iangalienamna ya kuweza kuwasaidia wasanii hao.

Theo Walcott: Arsene Wenger '99%' ANASAINI KANDARASI MPYA

Theo Walcott

Kocha wa Arsenal Raia wa ufaransa  Arsene Wenger amesema  "99%" anauhakika kuwa mshambuliaji wake  Theo Walcott atasaini kandarasi mpya klabuni hapo mwishoni mwa juma hili ambapo mambo yatakuwa yamekamilika Walcot  23, ambaye yupo katika miezi sita ya mwisho klabuni  hapo na anao uwezo wa kuondoka wakati wa kiangazi.

Laki ni wenger amesema kuwa kwa sasa ana asilimia 99 za kumbakisha mchezaji huyo .
"sikuwa na furaha pale niliposkia angeondoka "
"Imetuchukua muda kufika  hapa tulipotaka bado hatujalimaliza lakini itakuwa tayarai ndani ya juma hili" .
Walcott ndio mfungaji anaeongoza kwa arsenal akiwa amefunga magoli  14 .
Mchezaji huyo alikataa kandarasi ambayo angepewa ujira wa pauni  £75,000 lakini yeye alitaka kulipwa pauni laki moja kwa juma

Wenger bado anahusishwa  na kutaka kumsajiri winga wa  Crystal Palace  Wilfried Zaha, Mchezaji huyo Mwenye miaka 20 Aidha  mfaransa huyo amethibitisha kutaka kumsajiri mchezaji  , Taarifa zinasema kuwa Arsenal wako mbioni kumsajiri  mshambulijai wa Napoli mwenye miaka  25-Kutoka Uruguay   Edinson Cavani. 
huku akisema bei inaweza kupanda na ni jambo la kawaida  lakini inaweza kupungua siku za mwisho au saaa kdhaa kabla dirisha kufungwa.

Bolton Wanderers' Bulgarian midfielder Martin Petrov scores his penalty against Wolves

Petrov AMALIZA UHAMISHO WA KWENDA  Espanyol

Martin Petrov Amekamilisha uhamisho wake kutoka katika klabu ya  Bolton  Kuelekea  La Liga hasa katika klabu ya  Espanyol, Klabu hiyo  inayoshiriki ligi ya pili nchini uingereza imethibitisha 

Kocha wa Botlon  Dougie Freedman amekumbusha kuwa mchezaji huyo kutoka  Bulgaria alikuwa akifanya mazungumzo  mapema wiki hii na  Barcelona-lakini mazungumzo hayo yamekamilika Rasmi kwa kujiunga na Espanyol 

Petrov aliwahi kuchezea Nchi  USpania  akiwa na  Atletico Madrid kabla hajakwenda  Manchester City majira ya kiangazi   2007.

SUPERSPORT WIKI TENA VPL


 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4k2la-rrTsi6yk3pnVaxA5XS4NWf4rAJAmcuVKq_KKVhbF0TWRA8VK2X6rcl52PKbDGkDErR2yut7TyV5jtovTYNiGNOgX1OLS9JW0z1uYRUE7zEBuPy0Mq7dSZJiyd9Nujfji31mHDQ/s1600/SS9E+Logo+white.PNG
Mzunguko wa pili ya Ligi Kuu ya Vodacom utaanza Januari 26 mwaka huu huku kukiwa na maombi ya televisheni ya SuperSport kuonesha mechi za Super Week kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.

Raundi tano za awali katika ratiba ya mzunguko wa pili zinabaki kama zilivyo wakati nyingine zilizobaki zitatolewa baada ya kuingiza mechi za Super Week.

Wakati huo huo, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza unatarajia kuanza Januari 26 mwaka huu. Ratiba ya ligi hiyo na tarehe rasmi ya kuanza itatangazwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayotarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki.

HAPATOSHI TFF 56 WAPIGANA VIKUMBO KWENYE FOMU

 


Wakati kesho ndiyo mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) waombaji 36 wameshachukua na 18 tayari wamesharejesha.

Idadi hiyo ni kufikia leo mchana (Januari 17 mwaka huu). Pia Kamati ya Uchaguzi ya TFF inasisitiza kuwa wanaorejesha fomu hizo kwa email wanatakiwa kuzituma kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa email ya tfftz@yahoo.com na si kwa email binafsi za wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi au maofisa wa TFF.

Waombaji wanne walioongezeka katika orodha ni Blassy Kiondo kwa Kanda ya Katavi na Rukwa, Eliud Mvella (Mbeya na Iringa), Geofrey Nyange (Morogoro na Pwani), na Omari Abdulkadir kwa Kanda ya Dar es Salaam.

Orodha kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais) wakati waombaji wa umakamu wa rais mpaka sasa ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.

Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).

Athuman Kambi na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala na Eliud Mvella (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).

Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.

NAKARIBIA ULAYA SASA!!!


 http://kandanda.galacha.com/wp-content/uploads/2013/01/emmanuel-okwi_3601.jpg

 Mshambuliaji mpya wa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia, Emmanuel Okwi, amesema kwamba kusajiliwa kwake na klabu hiyo ambayo ni moja ya klabu vigogo barani Afrika ni dalili njema  na anaamini kuwa sasa amebakiza hatua chache kuufikia mlango wa kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Simba imemuuza kwa Etoile mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda kwa dau la dola za Marekani 300,000 (Sh. milioni 470). Etoile ni mabingwa wa Afrika mwaka 2007.

  Amesema  kwamba sasa anaiona Ulaya iko karibu zaidi kwake na kwamba, anachotakiwa kufanya ni kuendelea kucheza soka kwa kiwango cha juu na kuzingatia nidhamu ya mchezo huo.

Okwi amesema kuwa baada ya kukosa timu Austria mwaka jana,  kamwe hakuweza kukata tamaa na anamshukuru Mungu kwamba ubingwa wa mashindano ya Kombe la Chalenji yaliyomalizika mwaka jana jijini Kampala ulimsaidia kuimarisha kiwango chake na kwenda kwenye majaribio akiwa fiti.


"Ewe Mungu, nakushukuru kwa kuniwezesha kutimiza malengo yangu katika kiwango cha juu, bila ya wewe nisingeweza kufika hapa nilipo sasa," aliongeza Okwi, akirejea kile alichoandika juzi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook.


Nyota huyo aliyezaliwa Desemba 25 mwaka 1992, aliongeza kwamba kila anachokifanya na hatua anazizifikia katika kucheza kinatokana na juhudi zake na maombi anayoyafanya kila anapomaliza mazoezi.



Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, ndiye aliyekwenda Tunisia kukamilisha mazungumzo ya kumuuza mchezaji huyo na kusema kwamba tayari taratibu za uhamisho zimekamilika.

Rage amesema  kuwa katika mkataba ambao Okwi amesaini, Simba itaendelea kufaidika ikiwa Mganda huyo atauzwa kwa klabu nyingine.

Mgombea mmoja wa uchaguzi TFF kazaliwa 1952 sokondari kamaliza 1992

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Deogratius Lyato ameanika 'madudu' yanayofanywa na baadhi ya watu wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo uliopangwa kufanyika Februari 24.

Akizungumza wakati wa semina ya wahariri na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi huo iliyofanyika kwenye ofisi za makao makuu ya shirikisho hilo , Lyato amesema kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakigushi vyeti vya elimu na wengine kutumia vyeti vya watoto wao na ndugu zao.


“Tunakumbana na vituko vingi vya ajabu kwenye mchakato wa uchaguzi. Mgombea mwingine amezaliwa mwaka 1952, lakini anakuja na cheti kinachoonesha kwamba amehitimu elimu ya sekondari 1992. Unajiuliza, ilikuwaje?” .


“Baadhi ya wagombea wanakuja na vyeti vya watoto au ndugu zao kwa sababu tu majina yao yanakaribiana. Katika  mazingira kama haya, kamati inalazimika kufanya kazi kwa umakini mkubwa kwa sababu tunaamini hakuna kitu kigumu kama kudanganya. Tunawanasa kirahisi sana,” aliongeza.


Mwenyekiti huyo aliongeza  kuwa kamati yake inafanya kazi kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali kuhakikisha kuwa wanapata watu sahihi.


“Kila anayeleta cheti cha elimu, tunawasiliana na shule na vyuo alivyosoma na hata Necta (Baraza la Mitihani la Taifa). Tunafanya hivyo kwa sababu kuna watu wengi wanataka waingie katika uongozi wa shirikisho hili ilhali hawana sifa zinazotakiwa,” .


Katika semina hiyo iliyohudhuriwa na wahariri na waandishi wa habari zaidi ya 40, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah aliwakumbusha wanahabari hao kuhusu uandishi wa habari wenye weledi kuhusiana  na uchaguzi huo.

 


lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers