HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

16 March 2014

MALARIA YAUA BONDIA TANZANIA .Bondia wa ngumi za kulipwa Fadhili awadh amefariki dunia katika hospital ya mwananyamala baada ya kuugua kwa siku kadhaa.
 Fadhili awadh alikuwa ni miongoni mwa mabondia waliochaguliwa kucheza  mpambano wa ubingwa tarehe 29 mwezi huu  dhidi ya mpinzani wake toka tanga Alan Kamote, hivyo pia alikuwa katika maandalizi ya mpambano huo. Sababu ya kifo chake kwa ripoti ya daktari wa mwananyamala kwa kiongozi wa ngumi Ibrahim Kamwe ni kuwa fadhili alikuwa na malaria na alitumia dozi ya metakelfin, na hali ilibadirika pale alipojaribu kufanya  mazoezi na kujisikia vibaya na kuwahishwa katika hospitali hiyo ambayo alikaa kwa siku mbili akiendelea na matibabu na hatimae umauti ulipomkuta. Fadhili awadh mwenye umri wa maika 32 alikuwa anaendelea vizuri katika mchezo huo kiasi cha kufikia kucheza pambano la ubingwa katika ukumbi wa PTA sabsaba, akiwasindikiza mabondia japhet kaseba na Thomas mashali .
 sisi tulimpenda lakini mungu alimpenda zaidi ,Ailaze roho ya marehemu Fadhili awadh “tiger” peponi,shughuli za maazishi zinafanyika nyumbani kwao maeneo ya manzese.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers