HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

15 March 2014

MVUA YAHARIBU PAMBANO LA MTIBWA NA YANGA VPL

 




Klabu ya soka ya Yanga leo imetoka suluhu bila kufunga (0-0 ) dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar ya Manugu mkoani Morogoro  katika mchezo uiofanyika katika  dimba la Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


Young Africans ikicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu kwa takribani wiki mbili baada ya kutolewa katika mashindano ya kimataifa iliwakosa wachezaji wake wanne mlinda mlango Deo Munish "Dida" ambaye ni majeruhi, Mbuyu Twite (ruhusa), Haruna Niyonzima (malaria) na Mrisho Ngasa (majeruhi). 

Katika mechi ya leo mjini Morogoro, mchezo ulikosa radha kwa timu zote kutokana na mvua kubwa zilizoyesha mjini Morogoro na kusababisha wachezaji kushindwa kuonyesha ufundi wao na kujikuta mara nyingi wakiteleza na kukosa mipira au mipira kuwapita na kutoka nje.

Washambuliaji wa Young Africans walifanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Mtibwa Sugar kupitia kwa washambuliaji wake Emmanuel Okwi, Didier Kavumbagu, Saimon Msuva na Hamis Kizza lakini walikuta mipira yao ikiokolewa na walinzi wa Mtibwa Sugar na mingine  kutoka meta kadhaa pembeni ya lango.

Dakika ya 82, 84, 87, 89 na 90 Young Africans ilikosa nafasi za wazi za kuweza kujipatia bao kupitia washambuliaji wake Okwi, Didier na Javu baada ya mipira waliyoipiga kuokolewa na golikipa Sharrif Husein  na mwingine kugonga mwamba na kutoka nje na  kona ambazo hazikuzaa matunda.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Mtibwa Sugar 0 - 0 Young Africans.

Aidha kwa upande wa Mtibwa mchezaji Abdallah Juma alizawadiwa kadi nyekundu kwa kosa ambalo bado halikuoneka kirahisi  
AZAMA COMPLEX 
Azam fc 4-0Coast union 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers