Mwanamuziki maarufu wa mtindo wa Pop, Michael Jackson amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 50. Imeelezwa alipata matatizo yanayodhaniwa kuwa ya moyo.
Mwanamuziki maarufu wa mtindo wa Pop, Michael Jackson amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 50. Imeelezwa alipata matatizo yanayodhaniwa kuwa ya moyo. Mwanamuziki maarufu wa mtindo wa Pop, Michael Jackson amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 50. Imeelezwa alipata matatizo yanayodhaniwa kuwa ya moyo


Madaktari wa huduma ya kwanza walijaribu kuuzindua moyo wa Jackson wakati gari ya wagonjwa ilipokuwa ikimkimbiza katika hospitali ya UCLA, maafisa wameeleza.
Makundi ya watu, wengi wao wakiwa mashabiki wake wamekuwa wakikusanyika nje ya hospitali hiyo, ambako kituo cha wagonjwa wa dharura kimezungushiwa utepe na polisi na baadhi ya barabara kufungwa.
Jackson alikuwa akitarajiwa kuanza matamasha mbali mbali ya kufufua kipaji chake kwenye ukumbi wa O2 jijini London ifikapo tarehe 13 Julai.
Imeelezwa alikuwa na historia ya matatizo ya kiafya na hajawahi kukamilisha ziara ya matamasha kwa kipindi cha miaka 12 iliyopita

No comments:
Post a Comment