17 July 2010

JAMANI KISWAHILI NI BORA HATA BBC KINATUMIKA

Msanii wa Tansia ya Filamu Bw.Steven Kanumba. Leo ni Swahili dei ya ziff 2010, katika mkutano na waandishi wa habari Visiwani Zanzibar Kanumba na Ray walilia lugha ya kiswahili iendelee kutumika zaidi ilikukuza soko la filamu na lugha kiswahili,Kanumba aliwataka wasanii wakienzi kiswahili ili kukikuza kimataifa ambapo walitaka kila mwaka kuwe na midahalo ya mara kwa mara kuhusiana na wizi wa filamu,jambo hii lilifanya baadhi ya watu kuguna na kusema kuwa jamaa maimuna kimya kimya!! Wasanii hawa wa Tansia ya Filamu walisema kuwa seriakli imelala hivyo wanatakiwa kuzinduka ili kumkomboa mtanzania “tunaamua kutoa filamu za part one na two ilikujipatia kipato lakini kama tusipo fanya hivyo tutalala njaa! alisema kanumba alipokua akijibu swali la waandishi wa habari. Kwa upande wa Ray Kigos alisema kuwa wao hawakopi wala kuiga kutoka naigeria ila wanachokifanya wao ni kuhakikisha wainatunga filamu zilizo na mahadhi ya Kiafrika “nashangaa wanasema tunaiga naigeria wakati huko na huku kila kitu sawa ila wao wametangulia” alisema Ray. ZIFF 2010 ambayo ni msimu 13 tangu ilipoanza wasanii Ray na Kanumba ni mara yao ya kwanza kuhudhuria kama mastaa wa filamu za Tanzania ambao wote ni waigizaji,waongozaji na waandaaji. Wasanii ambao wapo Zanzibar kuhudhuria tamasha la ZIFF ni pamoja na mzee C\hilo, Monalisa, Haji Adam “baba adamu’ au mzee wa hisia, na wengine wengi tamasha ilo linatarajiwa kufungwa kesho jioni. Mohamed dweji blogspot. undestanda

No comments:

Post a Comment