HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

6 September 2010

MPIRA WA PETE AFRIKA KUSINI WAIONA

TANZANIA imeanza vyema mashindano hayo kwa kushinda mechi yake ya kwanza kwa magoli 50 kwa 25 dhidi ya Lesotho. Akifungua mashindano hayo naibu waziri wa michezo wa AFRIKA KUSINI GERT OOSHIZEN amesema kuwa mashindano hayo yanaimarisha mchezo huo na kuweka uhusiano mzuri baina ya nchi zinazoshiriki. Mchezo mwingine ulikuwa kati ya ZIMBABWE na AFRIKA kusini ambapo timu hizo zimeonyeshana kazi kubwa kutokana na kila timu kujiandaa vilivyo ambapo AFRIKA KUSINI iliibuka mshindi kwa magoli 64 kwa 29. Kwa upande wake kocha wa TANZANIA SIMONE MCKIWIS amesema mefurahia ushindi wa timu yake na kuahidi watanzania kuwa timu hiyo itaendeela kufanya vizuri katika michezo yake inayoendeela ambapo amewataka watanzania kuiunga mkono timu hiyo. Hata hivyo mashindano hayo yamekosa msisimko mkubwa kutokana na mashabiki wachache kuhudhuria, tofauti na mashindano ya kimataifa yaliyofanyika nchini mwaka jana ambapo watu mbali mbali waliweza kuhudhuria. Mashindano hayo yanashirikisha timu sita kutoka AFRIKA ambazo ni NAMIBIA, TANZANIA, BOTSWANA, LESOTHO, ZIMBABWE, na wenyeji AFRIKA KUSINI.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers