1 April 2011

PESA ZA MWAGA TAIFA STARS

MKUTANO MKUU WACHANGIA STARS Timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo inashiriki michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazochezwa Gabon- Equatorial Guinea mwakani imechangiwa sh.milioni moja laki tisa na themanini elfu Fedha hizo kwa Taifa Stars iliyo kundi D pamoja na Morocco, Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati zilichangwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliofanyika Machi 26 na 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Mkutano huo walishuhudia mechi kati ya Taifa Stars na Jamhuri ya Afrika ya Kati iliyochezwa Machi 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Walichanga fedha hizo kuipongeza Stars baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment