24 August 2012

BARCELONA 3-2 REAL MADRID MKONDO WA KWANZA SUPERCOPA

Cristiano Ronaldo, Dani Alves - FC Barcelona v Real Madrid


Barcelona imeitandika kwa mara ya kwanza katika msimu huu  Real Madrid katika vita  ya kuwania ufunguzi wa ligi ya soka ya uispania  maarufu kama supercopa, Baada ya kuibuka na ushindi mdogo wa mabao matatu kwa mawili katika uwanja wa  Nou Camp usiku wa kuamkia leo  ambapo kipindi cha kwanza timu zote zilijaribu kumiliki mpira lakini vijana wa Jose Mourinho's walijitahidi kuonyesha ukakamavu baada ya kuto kuruhusu goli katika kipindi cha kwanza. Lakini mpira ulibadilika kabisa katika dakika ya 55 baada ya  Cristiano Ronaldo' kuwapa wageni goli la kuongoza akiunganisha mpira wa kona lakini haikuchukua muda kwani dakika moja baadae  Pedro,alisawazisha kabla lionel Mesi kufunga kwa pernaty iliyotokana na Xavi Hernandez kufanyiwa faulo  katika eneo la hatari  ujinga uliofanywa na kipa wa Barcelona, Victor Valdes  kushindwa kukoa mpira uliopigwa na beki wake kwa kumrudishia pasi  ilikuwa ni zawadi kwa Ange Di Maria aliyekwamisha mpira wavuni katika  dakika ya 78 Xavi hernandez aliipatia barca goli safi kabisa ndani boksi na kuifanya barcelona kushinda mechi hiyo sasa timu hizo zitarejeana wiki ijayo katika uwanja wa Santiago  Bernabeu huku real ikihitaji ushundi wa mabao mawili sifuri ili itwae taji hilo .

No comments:

Post a Comment