5 August 2012

MANJI ALA KIAPO LEO

Mwenyekiti wa klabu ya yanga yusph manji akiapishwa na moja katika ya wazee wa baraza mbele ya Mama Fatma Karume





MKE wa rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amaan Karume, Mama Fatma Karume leo amwaapisha viongozi wapya wa Yanga, waliochaguliwa Julai 15, katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Walioapishwa katika zoezi hilo lililofanyika makao makuu ya klabu, makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani ni Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu wake, Clement Sanga na wajumbe watatu, George Manyama, Aaron Nyanda na Mussa Katabaro, wakati Abdallah Bin Kleb yuko kwa majukumu ya klabu mjini Kigali, Rwanda, yeye ataapishwa baadaye.
Aliyekuwa akiwaapisha viongzi ni Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Dk Jabir Idrisa Katundu, ambaye pia Mjumbe wa Baraza la Wazee la klabu.

Mama fatuma karume akimpa mkono wa kheri mwenyekiti wa klabu ya yanga yusuph 


 Good luck Young afrcans

No comments:

Post a Comment