5 August 2012

MKUCHIKA AINGIA YANGA .

 
 
 
Aliyeko kushoto ndiye mkuchika
 
Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga inayokutana katika makao makuu ya klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake Yusufu Manji imemtangaza mheshimiwa George mkuchika kuwa mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamni wa klabu hiyo.
Uamuzi huo umetolewa na mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji katika mkutano wa kusimikwa rasmi madarakani kwa uongozi mpya wa klabu hiyo zoezi ambalo linaendelea katika makao makuu ya klabu hiyo chini ya mama mlezi wa Yanga mama Fatma Karume.
Sambamba na hilo kamati mpya ya utendeji ya klabu hiyo imeamua kufutilia mbali kamati zote ndogondogo ndani ya klabu hiyo kuanzia leo.
Katika kuhakikisha kuna kuwa na umoja zaidi katika maamuzi uongozi wa Yanga umesema utakuwa ukikutana na viongozi wa matawi kila mwezi kwa lengo la kubadilisha mawazo.

www.rockersports .com comfirmed

No comments:

Post a Comment