1 September 2012

TFF YATOA UFAFANUZI KUHUSU ADAM NDITI

 

Shirikisho la soka Tanzania (TFF),limetoa ufafanuzi kuhusu utaratibu  unaotumika kuhusu kumpata mchezaji wa klabu ya soka ya Chelsea Adam  Nditi ambaye ni Mzanzibar na Raia wa Tanzania kama anaweza kuchezea timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ambapo walijaribu kuwasiliana na klabu ya soka ya Chelsea ambako ndiko anaposukuma gozi katika timu ya Vijana , ilikutazama uwezekano wa kumpata mchezaji huyo . lakini klabu ya Chelsea iliijibu Tff kuwa lazima wawasiliane na klabu kwanza halafu ndio wapate ruhusa ya kuwasiliana Mchezaji huyo  , Afisa Habari wa Shirikisho la soka la Kandanda la Tanzania, Boniface Wambura amesema nia ya kumhitaji mchezaji huyo ni kutaka akutane na kocha kwanza iliwafahamu kama yeye mwenyewe anataka kuchezea timu ya taifa ya Tanzania au Vinginevyo kwani wanahofia kuwa wanaweza kumuita lakini tayari akawa hana mwamko wa kucheza timu ya taifa ya Tanzania au tayari ana Hati ya kusafiria ya Uingereza

SIKIZA HAPA :
 



No comments:

Post a Comment