7 September 2012

WACHEZAJI WAWILI WAOMBEWA ITC URENO



Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ureno (FPF) limetuma maombi kwa  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuipatia Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wawili waliokuwa wakicheza mpira nchini.
 
Wachezaji wanaoombewa ITC ni Hamis Thabit Mohamed (19) ambaye klabu yake ya mwisho aliyoichezea nchini ilikuwa African Lyon wakati mwingine ni Abuu Ubwa Zuberi (20) ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea timu ya Yanga.
 
Kwa mujibu wa FPF, wote wawili wanaombewa ITC kama wachezaji wa ridhaa (amateur) ili waweze kujiunga na timu ya Atletico Sport Clube ya Ureno ambayo haijawekwa bayana kama iko daraja gani nchini humo.
FPF imeomba kupatiwa hati ya maelezo ya mchezaji (player’s passport) kwa kila mmoja ikiwemo taarifa za ushiriki wao katika mechi rasmi zinazotambuliwa na TFF wakiwa katika klabu zao hizo za zamani.

No comments:

Post a Comment