4 September 2012

Zanzibar yaupania ubingwa riadha Tanzania

MIKOA mitano ya Zanzibar imethibitisha kushiriki michuano ya Taifa ya mchezo wa riadha  itakayoanza keshokutwa Septemba 7, mjini Dar es Salaam.Katibu wa Chama cha Riadha Zanzibar (ZAAA) Khamis Gulam, amesema kuwa, michuano hiyo itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania, itadumu kwa siku tatu, na  washiriki wa Zanzibar wanatarajiwa kuondoka kesho.
Amesema kuwa, kila mkoa utakuwa na wanamichezo 16 na hivyo msafara wa watu 80 pamoja na viongozi.
 wanamichezo wa Zanzibar watashiriki michezo yote ikiwemo kukimbia, kurusha tufe, kisahani, mkuki na kuruka vihunzi.Gulam amesema kuwa anamatumaini  kuwa, Zanzibar itafanya vizuri na kwamba Mkoa wa Mjini Magharibi ambao ndio mabingwa watetezi, watatetea ubingwa wao.
 
.

No comments:

Post a Comment