HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

11 October 2012

Fabio Borini AVUNJIKA MGUU


Shikirisho la soka la italia FIGC Limethinbitisha kupitia tovuti ya Nchi yake kuwa mchezaji wa timu ya soka ya   Liverpool Mshambuliaji Fabio Borini amepata majereha katika mguu wake wa kulia . 

Borini, ambaye alikuwa akifanya mazoezi katika timu ya chini ya miaka ishirini na moja huku akijiandaa na mechi ya  kuwania fainali za kombe la dunia dhidi Sweden siku ya ijumaa alifanyiwa vipimo vya MRI na vimeonyesha kuwa amepata majeraha ya kuchubuka kwa mfupa ndani ya mguu wake , Habari hizo hazitakuwa Nzuri kwa Timu ya soka ya Liverpool hasa kwa mkufunzi wa timu hiyo   Brendan Rodgers,ambaye kwa sasa anamshambuliaji mmoja mwenye umri wa juu   Luis Suarez.

Mchezaji huyu mwenye miaka 21 ambaye alijiunga  Liverpool akitokea Roma Mwezi july  kwa ada ya uhamisho wa pauni  £10.5million. amewahi kucheza chini ya mkufunzi huyo akiwa swansea city katika mwisho wa msimu wa mwaka  2010-11 ambapo aliisaidia timu kupanda daraja   katika ligi ya premier ya uingereza Ambapo Swansea ilimsainisha mchezaji huyo kutoka Chelsea kwa mkopo , ambapo wao walimsainisha kutoka  Bologna mwaka  2007. Borini amecheza mechi kumi za  Liverpool  msimu huu na amefunga mechi  moja tu katika mashindano ya kufuzu michuano ya  UEFA Europa league Dhidi Gomel Mwezi  August.

kwa sasa liverpool ipo katika wakati mgumu tena baada kumtoa Andy Carroll kwa mkopo wa muda mrefu tena kwa mahasimu wao   West Ham, Rodgers anakabiriwa na sintofahamu hasa katika nafasi yake ya ushambuliaji na watapambana na dhidi ya READING katika mechi yao inayofuata katika ligi ya premier ya uingerza oktoba ishirini mwaka huu   . 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers