31 October 2012

Metzelder APATA MAJERUHI MAPYA


Mlinzi  wa  Schalke 04's na beki wa zamani wa Timu ya taifa ya Ujerumani  Christopher Metzelder ameumia tena nyonga katika mwanzo mwingine wa msimu wa ligi ya ujerumani na atakosa mechi nyingine jumamosi hii dhidi ya  Hoffenheim.

 Mchezaji huyo mwenye miaka 31-alitoka nje katika mechi ambayo timu yake ilishinda mabao matatu kwa sifuri dhidi timu ya ligi daraja la pili ya SV Sandhausen katika mzunguko wa pili wa kombe la ujerumani  DFB-Pokal hapo jana lakini haijafahamika atakuwa nje kwa muda gani  "Nina masikitiko ya kwakuwa nimetonesha msuli wangu katika sehemu ya nyonga ," Metzelder aliiambia tovuti ya klabu yake ya  Schalke's .

Schalke wataikaribisha Arsenal katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya siku ya jumanne , Metzelder, ambaye  amechezea mara  47 hasa katika michuano ya ulaya inayofahamika  kwa   UEFA EURO 2008 ambapo ujerumani ilicheza fainali  Dhidi ya Uispania na kufungwa goli moja sifuri  ,bado anapigana na muda na umri katika kuichezea klabu yake

Tangu ajiunge  Schalke akitokea Real Madrid Mwezi July 2010, Metzelder ameichezea mara   48 katika ligi ya ujerumani   Die Königsblauen, na amefunga magoli mawili .

No comments:

Post a Comment