HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 October 2012

MGOMBEA AGOMA KUHOJIWA NA BABA MKWE

Mjumbe wa Kamati ya uchaguzi aliyekataliwa na kulazimika kutolewa ndani ya chumba cha usaili ili haki itendeke kwa mgombea ni Katibu, Prince Mwaihojo, ambaye anadaiwa kuwa ni Mkwe wa mgombea mmoja wa nafasi ya Uenyekiti John Mwamwaja. 

USAILI wa wagombea wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama cha soka mkoa wa Mbeya, (MREFA), umegubikwa na vituko vya aina yake, baada ya mmoja wa wagombea wa nafasi ya Uenyekiti, kumkataa mjumbe wa kamati ya uchaguzi kwa madai kuwa ana mgongano wa kimasilahi na mpinzani wake.

Mjumbe wa Kamati ya uchaguzi aliyekataliwa na kulazimika kutolewa ndani ya chumba cha usaili ili haki itendeke kwa mgombea ni Katibu, Prince Mwaihojo, ambaye anadaiwa kuwa ni Mkwe wa mgombea mmoja wa nafasi ya Uenyekiti John Mwamwaja.

Katibu huyo wa Kamati ya uchaguzi, akitoka nje muda mfupi tu baada ya mmoja wa wagombea ya nafasi ya uenyekiti Elias Mwanjala, alipoitwa ndani ya chumba cha usaili.

Kwa upande wake, Mwaihojo alipoulizwa juu ya sakata hilo la kukataliwa, amekiri kuwa lilitokea na si la ajabu katika mahala popote ambapo haki inafuatwa, hivyo kitendo hicho hakizuii mchakato wa kuwapata viongozi wa chama hicho.

Akitoa taarifa ya mchakato wa zoezi hilo baada ya kumalizika, Mwaihojo alisema zoezi hilo la usaili kwa limefanikiwa kwa asilimia 90 kwa kuwa wagombea 14 walifanyiwa usaili na kubakiza wagombea wanne tu ambao watamalizia hawakufanyiwa.

Kwa mujibu wa Mwaihojo, wagombea wanne ambao hawajafanyiwa usali ni Katibu anayemaliza muda wake Lawrence Mwakitalu, Andongwisye Panja, Thomas Kasombwe Sinkwembe ambao wote walitoa udhulu kutokana na kukabiliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kusimamia mitihani ya kidato cha nne inayoendelea hivi sasa.

Uchaguzi wa MREFA unatarajia kufanyika oktoba 27, jambo litakalowezesha kupatikana kwa uongozi mpya utakaohudumu kwa miaka mine kama katiba ya chama hicho inavyoeleza.

Aliwataja watu waliojitokeza kuomba nafasi za uongozi kwa nafasi ya Mwenyekiti kuwa ni John Mwamwaja ambaye ni makamu Mwenyekiti wa uongozi unaomaliza muda wake, wakati wengine ni Majuto Mbuguyo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji katika Halmashauri ya

Pamoja na Elias Mwanjala ambaye katika uchaguzi Mkuu uliopita aligombea ubunge katika jimbo la Kyela na kuangushwa vibaya na mbunge wa sasa Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye pia ni Waziri wa Uchukuzi.

Makamu Mwenyekiti ni Omary Mahinya, wakati nafasi ya Katibu Mkuu, Lawrence Mwakitalu, anayemaliza muda wake,Suleiman Haroub na Redson Kaisi, ambapo Katibu Msaidizi ni William Mwamlima na nafasi ya Mkutano Mkuu wa Taifa Tahdeo Kalua na Danny Korosso.

Kwa upande mweka Hazina ni Asajile Kavenga, Uswege Luhanga, wakati wajumbe wa kamati ya utendaji ni Lwitiko Mwamndela, Thomas Kasombwe, Boniface Sinkwembe.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers