29 October 2012

SHIREFA YAPOINGEZWA NA TFF


 





Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu).
 
Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SHIREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Shinyanga.
 
TFF imeahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya SHIREFA ambayo imechaguliwa chini ya uenyekiti wa Benester Lugora.
 
Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani  Shinyanga kwa kuzingatia katiba na SHIREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
 
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya SHIREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
 
Viongozi waliochaguliwa ni Benester Lugora (Mwenyekiti), Nassoro Said (Katibu Mkuu), Bivin Kapufi (Katibu Msaidizi), Mbasha Matutu (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF) na Michael Kaijage (Mwakilishi wa Klabu TFF).

No comments:

Post a Comment