5 November 2012

ABEID AYEW PELE AZALIWA TENA TANZANIA ATIMIZA MIAKA 48 AKIWA KWENYE ZIARA TANZANIA


Picha Pallangyor.blogspot.com/
Gwiji  wa soka barani Afrika Abeid Ayew Pele leo amesheherekea siku yake ya kuzaliwa nchini Tanzania.
 Pele ambaye pia ni balozi wa heshima wa FIFA yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kuhamasisha soka hasa la vijana akiwa na Ashford Mamelod na Emanuel Maradas walitembelea kituo cha soka cha Azam ambacho kipo Chamazi nje ya jiji la Dar es Salaam.
 Akiwa huko ghafla alishtukizwa kwa kuimbiwa wimbo wa happy birthday na keki iliyopambwa mithili ya uwanja wa soka (Mpira) wenye magoli ambayo aliandaliwa na uongozi wa Azam
 Pele mwenyewe alifurahi kwa kufanyiwa sherehe ya kuzaliwa kwake ambapo leo ametimiza miaka 48 ya kuzaliwa kwake.
 

No comments:

Post a Comment