6 November 2012

HUWEZI AMINI RONALDO NDIO SHUJAA WANGU:MESSI

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona  Lionel Messi, amekiri kuwa  mchezaji anayevutia na amekuwa akijifunza kwake ni  Ronaldo kutoka brazil na sio huyu wa ureno
"Ronaldo alikuwa shujaa wangu ," Messi alinukuliwa katika jarida moja la kiingereza linalojulikana kwa mfumo wa  4-4-2 ,huku akimtolea mfano  MBrazili Ronaldo Luis Nazario de Lima, na sio mpinzani wake anayechezea Real Madrid's Cristiano, ambaye anapewa nafasi kutwaa tuzo ya FIFA Ballon d'Or.

"Nimetazama wachezaji kama  [Zinedine] Zidane, Ronaldinho na Rivaldo lakini  Ronaldo ndio mshambuliaji ambayo sijaona anayefanana nae  ," aliongeza kwa kusema . "alikuwa na kasi sana alikuwa anaweza kufunga popote na alikuwa anaweza kupiga mpira kuliko mtu yeyote ambaye sijawahi kuona ."

Messi, 25, ni moja kati ya wanandinga  23  katika orodha ya wachezaji wanaonia tuzo ya uchezaji bora maarufu kama FIFA Ballon d'Or . kama  Ronaldo, ambaye pia aliwahi kucheza Barcelona, na Gwiji la soka toka ufaransa   Zidane, ambao na wamewahi kushinda tuzo hiyo mara tatu.  

No comments:

Post a Comment