11 November 2012

JUVE ,CLAAx2 CLAAX2JUVEEEE


Ikicheza mechi ya  50th ya ligi ya Nyumbani bila kufungwa huku ikichagizwa na ushindi wa bao nne sifuri dhidi   4-0 ya  Nordsjaelland katika ligi ya Mabingwa ulaya jana ilifanya kufuru tena , baada ya kuifumua   Pescara 6-1 na kuongoza ligi hiyo kwa alama nne kileleni katika ligi ya  Serie A.

Inter Milan waliziba pengo hilo kwa alama moja baada ya ushindi wa mabao matatu siku saba zilizo pita lakini kazi itakuwa nzito leo watakapo safiri kuifuata  Atalanta ambayo inashika nafasi za kati katika ligi ya italia .

Mshambuliajai wa Juve  Fabio Quagliarella akichagizwa na goli alilofunga katika ya wiki dhidi ya timu kutoka Denmark alifunga mabao matatu  Sebastian Giovinco naye alifunga bao moja .

Arturo Vidal, ambaye alifunga goli katika mechi zote mbili kati Inter na Nordsjaelland, naye alifunga goli lake la nne katika mechi nne mfululizo   Kwadwo Asamoah  naye alifunga kwa kichwa  na kumaliza kalamu ya goli sita -- Goli la  Pescara's lilifungwa na  Emmanuel Cascione.

No comments:

Post a Comment