20 November 2012

Mark Hughes HAJAFUKUZWA


Kocha wa Queens Park Rangers  Mark Hughes, anabakia na kibarua chake cha kupasha mawaidha katika klabu hiyo baada ya kukutana na mkuu wa klabu hiyo Philip Beard.

 Taarifa zilisema kuwa Mkufunzi  huyo wa zamani wa  Wales alifukuzwa baada kukutana  na mkuu huyo katika viwanja vya mazoezi  .
Hughes anafanya kazi akiwa katika uangalizi baada ya Timu hiyo  kutopata ushindi tangu ligi ya premier ianze na inashika nafasi za mwisho katika msimamo wa ligi ya uingereza  baada ya kucheza mechi kumi na mbili bila kushinda hata mechi   lakini moja ya wawakilishi wa klabu hiyo  Kia Joorabchian alisema  taarifa  hizo sio za kweli bali zilikuwa ni za uzushi mtupu .

No comments:

Post a Comment