HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

6 December 2012

UGANDA VS KENYA CECAFA FINAL


Timu ya soka ya taifa ya Kenya imeifunga Zanzibar katika mapigo ya penati na kufuzu hatua inayofuata ya mashindano ya Cecafa yanayaofanyika Uganda 
Harambee Stars walitoka nyuma mara mbili na kuapata suluhu ya mabao mawili kwa mawli na kupereka mpira katika dakika za nyongeza ambapo timu hizo zilishindwa kufungana pia katika daika hizo 

 Khamis Mcha Khamis aliipatia  Zanzibar goli la  uongozi katika dakika 21 lakini dakika chache baadae Mlinzi wa timu taifa ya Zanzibar   Nadir Haroub aliokoa mpira vibaya na kujifunga na kufanya mpaka nusu ya kwanza kwenda sare ya bao moja kwa moja.



Zanzibar ilipata tena goli la uongozi kwa goli lililofungwa na  Aggrey Morris katika dakika ya  76th ,lakini dakika nne kabla mpira haujamalizika   Mike Baraza aliisawazishia kenya goli la pili .

 Timu zote mbili zilimaliza mechi zikiwa na wachezaji kumi wakati mcheza wa timu ya taifa ya Zanzibar's Ahmed Adeyom alionyeshwa kadi ya pili ya manjano baada ya kumfanyia madhambi  Victor Ochieng, aliyeingia kipindi cha pili na  alishindwa kuendelea na mchezo  baada ya kupata maumivu makali .

 lakini bahati ya robo fainali haikuweza kuendelea kwa Zanzibar katika upigaji wa penati  ambapo walishindwa kufunga penati mbili , wakati  Mike Baraza, Joackins Atudo, Edwin Lavatsa na  Abdalla Juma wote walifunga penati zao kwa upande wa Kenya.

 Bingwa mtetezi   Uganda, katika mchezo uliofuata  waliiibaamiza , inavyotakiwa  Tanzania Bara  3-0 katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya CECAFA

 Magoli mawili yaliyofungwa na Robert Ssentong na moja likifungwa na mshambuliaji wa klabu ya simba Emmanuel Okwi yaliiipa siku ya furaha  Timu ya taifa ya uganda na kujihakikishia kucheza fainali kwa mwaka 2012 katika mashindano ya cecafa  .

 Jumamosi itakuwa ni marejeo ya fainali ya mashindano ya cecafa ya mwaka 2008 pale uganda ilipoifunga ndugu zao wa jadi kenya  goli moja  1-0.

 Zanzibar itacheza na ndugu zao Tanzania Bara katika kutafuta mshindi waa tatu  mechi itakayochezwa mapema zaidi .





No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers