HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

28 August 2012

MUSONYE AITOLEA NJE KENYA KUANDAA CECAFA ASEMA WALISHINDWA KUONGEA NA MDHAMINI


 Katibu mkuu wa Baraza la vyma vya soka afrika mashariki na kati  Nicholas Musonye Akipokea Kombe ambalo hushindaniwa kutoka kampuni ya  EABL (Uganda ) Ambaye ni mkurugenzi wa masoko  Lemmy Mutahi  katika sherehe iliyofanyika nchini uganda leo hii . kutoka kulia ni Makamu  rais FUFA Livingstone Kyambadde.

Je kwanini Kenya imepokonywa uenyeji wa kombe la chalenge.
SIKIZA HAPA:


Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya tusker ya uganda  Lemmy Mutahi  (katikati ) akikabidhi mfano wa hawala kwa Katibu wa baraza la vyama vya soka afrika mashariki na kati CECAFA Nicholas Musonye.Kulia  makamu wa rais wa  FUFA t Livingstone Kyambadde jijini kampala leo 

LUKA MODRIC AFUNGUKA KUHUSU UWEPO WAKE MADRID


Luka Modric 



  • kuzaliwa: 9 September 1985, Zadar
  • Dinamo Zagreb: 2003-2008 (112 alicheza , 31 goli)
  • Zrinjsku (Mkopo): 2003-2004 (22 appearances, eight goals)
  • Inter Zapresic (Mkopo): 2004-2005 (18 appearances, four goals)
  • Tottenham: 2008-2012 (160 alicheza, 17 goals)
  • Croatia alicheza : 58 (6 goli)  
Pichani ni kiungo wa mpya wa Klabu ya  Real Madrid amesema kuwa anajua itakuwa ngumu kwake kucheza katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid lakini anaamini kuwa ubora wake ndio utakaomfanya acheze kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
SIKIZA HAPA :

OLE WAKE ATAKAE THUBUTU !



 Klabu ya soka ya Dar es salaam yanga african kupitia kwa msemaji wake mkuu imesema yoyote atakaye husika kumgusa au kutaka kumfanyia chochote kile mchezaji wa timu hiyo raia wa jamhuri ya kidemokarisia ya watu wa kongo Mbuyu Twite atakiona kilichomtoa kanga manyoa, siku atakayo wasiri mchezaji kutokea nchini Rwanda ambako anakamilisha baadhi ya  taratibu kabla hajafika jiji dar es salaam tua jiji dar es salaam. nilipata bahati ya kukutana na Louis Sendeu ambaye ndiye mwenye dhama ya kuzungumza kwa klabu hiyo naye alikuwa na haya ya kusema kuhusu mchezaji huyo
SIKIZA HAPA 


KAMATI YA SHERIA KUPITIA USAJILI SEPT 2

Alex Mgongolwa Mwenyekiti wa kamati ya sheria Tff




Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2012/2013.
  Usajili utakaopitiwa ni wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Lidi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo Kamati itapitia pingamizi zilizowasilishwa na klabu mbalimbali dhidi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu zingine.Taarifa hiyo imetolewa na afisa habari wa shirkisho la mpira wa miguu tanzania tff Boniface wambura.

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers