HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

28 May 2013

HIZI NDIZO TETESI TU ZA KIFO CHA NGWEA HATARI TUPU !!!

 
mwanamuziki wa kizazi kipya anayefahamika kwa jina la kisanii Ngwea amefariki dunia leo asubuhi nchini afrika kusini Taarifa ambayo imezipata kutoka Afrika ya Kusini kwa HusseinOriginal ambaye yupo Pretoria, amesema Ngwear amefariki leo asubuhi kwenye gheto ambalo alikuwepo pia msanii M to The P ambaye yeye amelazwa hospitali akiwa mahtuti. 

"Tulivyokwenda kuwagongea asubuhi tuliwakuta Ngwear amefariki na M To The P akiwa amepoteza Fahamu Kabisa"

Baada ya kuwapeleka hospitali Daktari alitibitisha amekufa na ameshatoa taarifa kwa watu wa Karibu wa Ngwear huko Afrika nya Kusini.

Ngwea akiwa na msanii M to the P walitakiwa kurudi Dar leo lakini waliwakuta wamezimia kwenye chumba wote wawili baada ya kuzidisha (overdose) madawa ya kulevya na M to the P.

Hata hivyo mama yake Ngwear ambaye yupo nyumbani kwao Morogoro amethibitisha kupokea taarifa ya kifo cha mwanae na kusema kuwa taarifa za kuwa za kuwa alikuwa Afika ya Kusini alikuwa hana kwani mara ya mwisho kuongea naye zimepita wiki mbili sasa.

Pia amesema taratibu za maandalizi ya mazishi yatakavyokuwa yataanza baada ya kufika baba yake mdogo Ngwear ambaye yupo mkoani Ruvuma kwani anatarajiwa kuwasili kesho Morogoro.

Pia

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers