HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 January 2013

BINTI ABARIKI USHINDI WA AZAM MAPINDUZI CUP


AZAM FC Imefanikiwa kutetea Kombe la Mapinduzi usiku WA Kuamkia Leo  kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar baada ya kuifunga Tusker FC ya Kenya mabao 2-1.

Kwa ushindi huo, Azam wamezawadiwa Sh. Milioni 10, wakati washindi wa pili Tusker wamepata Sh. Milioni 5.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ramadhan Rajab Ibada ‘Kibo’ aliyesaidiwa na Mwanahija Makame Mfumo na Mgaza Kindundi, hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.



 Gaudence Mwaikimba alipewa pasi nzuri na Brian Umony dakika ya 44, lakini shuti lake kali lilidakwa na kipa Samuel Odhiambo.

Kipindi cha pili, Tusker walirudi na moto mkali na kuanza kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Azam,

na iliwasaidia mabingwa hao wa Kenya kupata bao dakika ya 60, lililofungwa na Jesse Were aliyeunganisha kwa shuti kali  pasi ya Robert Omunok
, bao hilo halikudumu sana, kwani Azam FC walisawazisha dakika ya 72 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na beki Mkenya, Joackins Atudo baada ya beki wa Tusker, Luke Ochieng kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Katika dakika mbili za nyongeza baada ya kutimia  dakika 90 za mchezo huo, alijitokeza binti mwenye umri kati ya 14 na 16 na kukatiza uwanjani akitokea jukwaa la Urusi.
Refa alijaribu kumsimamisha, lakini aliendelea kukatiza Uwanja hadi nje ambako alipokewa na askari Polisi na kutolewa nje kabisa ya Uwanja. Mtangazaji wa Uwanja wa Amaan, Farouk Karim aliwatuliza mashabiki akisema binti huyo ametoroka hospitali ya ugonjwa wa akiri , iliyopo Kidongo Chekundu na tayari Polisi wamemkamata na kumrejesha huko. 
Hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1 na ndipo zikaongezwa dakika 30.
Gaudence Exavery Mwaikimba aliipatia Azam bao la ushindi dakika ya pili tu tangu kuanza kwa muda wa nyongeza baada ya kuwazidi nguvu na maarifa mabeki wa Tusker.

Bin zuberyblog


1 comment:

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers