HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

2 January 2013

Chelsea yabadili mawazo kwa Demba Ba.

Ba, mwenye umri wa 27, sasa amepewa ruhusa na klabu yake kuzungumza na Chelsea kuhusu uwezekano wa kusajili na klabu hiyo.

Demba Ba sasa atakosa mechi ya leo usiku dhidi ya Everton.

 kandarasi ya Demba Ba inamruhusu  kuzungumza na vilabu vingine ambayo viko tayari kulipa kitita cha pauni milioni saba .

Mshambulizi huyo kutoka Senegal, ambaye alijiunga na Newcastle kutoka klabu ya West Ham mwezi juni mwaka wa 2011, ndiye mchezaji wa pili aliyefunga magoli mengi  msimu huu.

Kufikia sasa demba ba amefunga jumla la magoli 13.

Wakati huo huo klabu ya Liverpool imesema kuwa imemsajili mshambulizi wa timu ya taifa ya Uingereza na Chelsea Daniel Sturridge.

Sturridge, mwenye umri wa miaka 23, anaaminika alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu hiyo mwezi uliopita kabla ya mwezi huu wa uhamisho wa wachezaji.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers