HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

7 January 2013

SAMATA NA ULIMWENGU KUREJESHWA NCHINI


 


Washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa klabu ya TP Mazmebe ya Jamahuri ya Kidemokrasia ya Kongo wako shakani tena kujiunga katika kambi ya timu ya taifa (Taifa Stars) iliyoanza kambi jijini Dar es Salaam jana kutokana na uwezekano wa kuwekewa ngumu na timu yao.
 
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, amesema kuwa tayari wameshajulishwa  kwamba Samatta na Ulimwengu walioitwa kikosini na kocha wa Stars, Mdenmark Kim Poulsen hawawezi kuungana na wenzao hadi shirikisho hilo litakapozungumza na uongozi wa Mazembe ili kupata idhini ya kuwatumia.
Stars imeingia kambini jana kujiandaa kwa mechi tatu za kimataifa za kirafiki, ikiwamo dhidi ya timu ya taifa ya Ethiopia.

Wote wawili waliwahi kukataliwa na Mazembe kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) iliyoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Chalenji) iliyofanyika Kampala, Uganda na hivi karibuni walishindwa pia kuichezea Stars dhidi ya Zambia baada ya kutua nchini wakitokea Kongo wakiwa majeruhi.

"Bado hatuna uhakika wa kuwapata Samatta na Ulimwengu… ila tumeanza harakati za kuwaleta kitambo na tayari Sunday Kayuni (Mkurugenzi wa Ufundi TFF) amekwenda Kongo kuwaombea ruhusa,” .

Akieleza zaidi, amesema kuwa kambi ilianza jana na kuwahusisha wachezaji wengine isipokuwa wa Simba, Azam na Mtibwa zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi, Zanzibar na Yanga ambayo iko ziarani Uturuki.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers