10 January 2013

SERGIO RAMOS BENCHI MECHI TANO BILA UGONJWA WOWOTE

Mlinzi wa Real Madrid  Sergio Ramos amepewa Adhabu ya Kufungiwa kwa mechi tano baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu hapo jana usiku katika michuano ya kombe la mfalme Ambapo timu yake iliifunga   Celta Vigo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uispania alipewa adhabu hiyo katika dakika ya  72 baada ya kupewa kadi ya pili ya manjano na kuonyesha ishara  kuwa mwamuzi hakumtendea haki pindi alipokuwa akitoka nje ya kiwanja .

Shirikisho la soka la Uispania limetangaza kuwa mchezaji huyo atatumikia adhabu ya mechi moja  nje  na atakosa mechi nyingine tano kwa mujibu wa Kifungu cha  94  RFEF's Cha nidhamu kinacho zungumzia maswala ya udhalilishaji kwa waamuzi  au mtu yeyote  .

Madrid ilishinda Mabao  4-0 na kufudhu hatua inayofuata ya robo fainali baada ya kushinda kwa jumla ya magoli   5-2 .

No comments:

Post a Comment