HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

6 January 2013

WASANII TANZANIA KUFUNGIWA KUIGIZA

 

 SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF) limekemea baadhi ya wasanii walioonyesha utovu wa nidhamu katika msiba wa  aliyekuwa msanii wa filamu nchini, Juma Kilowoko ‘Sajuki’.


Pia limesisitiza kuwa msanii atakaeripotiwa katika vyombo vya habari kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu atafungiwa kuigiza.

A Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba alisema amesikitishwa na kitendo cha wasanii kuacha msiba na kwenda kunywa pombe wakati msiba huo ni wa dini.

Alisema baadhi ya wasanii kuonyesha utovu wa nidhamu katika msiba wa marehemu Kanumba na wengine katika msiba wa Sajuki.

“Nasikitika kuona msanii hajitambui hata kidogo, yani anaacha msiba anakwenda kunywa pombe tena jirani na mahala pa msiba, jamani huu msiba ni wa dini, hivyo atakayeripotiwa vibaya katika misiba TAFF tutamfungia” .

Katika hatua nyingine amesema msiba huo ulitawaliwa na utani hali ya kwamba umewakutanisha watani wa makabila.

Msiba huo ulitawaliwa na utani baada ya kuwepo kwa wasanii wachekeshaji kama vile, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya fedha, Lucas  Mhuvile ‘Joti’ na wengineo wengi.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers