11 March 2013

FRAT AIBU TUPU YASHINDWA KULIPA KODI YA PANGO




CHAMA cha waamuzi nchini (FRAT) kimeondolewa kwenye jengo walilokuwa wamepanga kutokana na kushindwa kulipa pango

FRAT ambao walikuwa wamepanga kwenye jengo la National Housing Corparation (NHC) lillilopo barabara ya Morogoro Posta wameondolewa leo majira ya saa sita mchana na madalali.


Katibu wa FRAT Charles Ndagala amekiri kutolewa vifaa nje na kusema ni kweli wanadaiwa Shilingi milioni tano ambazo ni kodi ya miezi tisa.


"Ni kweli tunadaiwa na tumetolewa vifaa vya ofisi nje hivyo tunaangalia jinsi ya kuhifadhi vifaa vyetu", 

Hata hivyo hali ya ukata ndio inaikabili chama hicho kiasi cha kushindwa kulipa kodi kwani hakina vyanzo vya mapato.
Mmoja wa wanachama Jamhuri Swalehe akisaidia kupakia vifaa kwenye gari
 katibu huyo alionekana akipakia vifaa hivyo kwenye gari aina ya canter na kuvipeleka kwenye ofisi za Shirikisho la Soka nchini (TFF). Tunaendelea kufuatilia kuona nini kimejiri

No comments:

Post a Comment