14 March 2013

KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA ,HATUTAMSIKIA TENA

Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA limethibitisha kifo cha aliyekuwa afisa habari  wa baraza hilo Finny Muyeshi ambaye amefariki dunia jana jioni.
Akiongea na Rockersports katibu wa baraza hilo Nickolaus Musonye amesema kuwa baraza lake limesikitishwa na kifo cha afisa habari wake ambaye amekuwa mchapa kazi hodari ndani ya baraza hilo ambaye aliugua kwa muda mrefu na hatimaye jana akafariki dunia.
Musonye amesema kuwa mazishi ya Muyeshi yatafanyika wiki ijayo.
Amesema kwa CECAFA huo msiba mkubwa kwani alikuwa mstarabu na mwenye kujituma muda wote katika kazi yake na kwamba pengo lake ni kubwa katika baraza hilo.

No comments:

Post a Comment