Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka mshambuliaji Nsa Job wa
Coastal Union kuwasilisha maelezo yake juu ya madai kuwa alipewa rushwa
ya sh. milioni mbili ili asiifunge moja ya timu vigogo vya soka nchini.
Job
alikaririwa Aprili 3 mwaka huu na kituo cha redio cha Clouds FM katika
kipindi cha Amplifier kuwa alipewa kiasi hicho cha fedha na kiongozi wa
timu husika ili asiifunge katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, lakini
alipokea fedha hizo na kuifunga timu hiyo.
Baadaye
kiongozi huyo alikuwa akimtaka arejeshe fedha hizo. Pia TFF
imekiandikia kituo hicho cha redio kutaka nakala ya kipindi hicho ili
pamoja na maelezo ya mshambuliaji huyo vipelekwe katika Kamati ya
Nidhamu kwa ajili ya hatua za kinidhamu.
TFF
itachukua hatua kali dhidi ya Job iwapo hatawasilisha maelezo yake
kuhusiana na suala hilo, na imetaka wadau kutoa ushirikiano ili iweze
kupambana kikamilifu na vitendo vya rushwa kwenye mpira wa miguu.
No comments:
Post a Comment