HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

29 May 2013

BEKI WA ZANZIBAR HEROES ATUA SIMBA

 
MCHEZAJI wa klabu ya Miembeni SC na timu ya taifa ya Zanzibar, ‘The Zanzbar Heroes’ Adeyoum Saleh Ahmed, ni miongoni mwa wanasoka wapya waliojiunga na timu ya Simba SC ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuichezea msimu ujao.  
Tayari nyota huyo ambaye ni mtoto wa kocha wa makipa wa Miembeni SC Saleh Ahmed ‘Machupa’, yuko jijini hapa akijaribiwa katika mazoezi ya kikosi cha wekundu hao kinachonolewa na Abdallah Kibaden aliyemrithi Mfaransa Patrick Liewig ambaye amerejeshwa kwao.
Simba wanafanya mazoezi katika uwanja nwa Kinesi Urafiki jijini Dar es Salaam, ambapo Adyoum ni miongoni mwa wanandinga vijana wanaofanya majaribio ili kumridhisha Kibaden, ambaye alikuwa mshabuliaji mahiri wa timu hiyo miaka ya nyuma.
  baba mzazi wa beki huyo wa kushoto Saleh ‘Machupa’, alithibitisha kuwa, mwanawe alikuwa katika orodha ya wanasoka wanaotakiwa na wekundu hao tangu walipomuona kwenye mashindano ya Chalenji mwishoni mwa mwaka jana nchini Uganda. Adeyoum amekuwa beki tegemeo katika kikosi cha Miembeni, akiisaidia sana kurudi ligi kuu ya Zanzibar baada ya kuuza nafasi yake kwa Mundu msimu uliopita, na pia alichangia Zanzibar Heroes kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Chalenji yaliyopita mjini Kampala, Uganda.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers