HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

11 May 2013

HIKI NDICHO KIKOSI BORA ZAIDI CHA FERGUSON KUPATA KUTOKEA MAISHANI MWAKE XI

Kwa hakika hivi vimekuwa vikosi Bora zaidi  Hasa unapuzungumzia  XI Bora za Sir Alex Ferguson ambavyo amewahi kuvipanga kiwanjani .
Huwezi kupingana nae wala kuongeza jambo katika hili  ,Ukianza Na mlinda mlango mahili kiwanjani ambaye alikuwa mkali kiwanjani  Peter Schmeichel. ambapo mbele yake akiwa na ukuta imara ambao ulikuwa ukiongozwa na , Gary Pallister na  Steve Bruce ambao walitengeneza maelewano mazuri sana kiwanjani , ukuta ambao mwandishi wa makala hii anasema haujawahi kutokea .anasema mbali ya hapo sehemu ya kiungo ilikuwa hatari zaidi kwani kulikuwa na kijana hatari Paul Ince ambaye tulikuwa nyuma yake alikuwa anajua nini cha kufanya kiwanjani .
Mark Hughes alikuwa hatari zaidi kwani alikuwa na miguu yenye nguvu zaidi na alikuwa na uwezo wa kuchukua mipira huku pembeni akiwa na kijana mfaransa Eric Cantona’s ambae alikuwa na uwezo wa hali ya juu katika kupiga chenga na kumiliki mpira kikosi kilimaliza ukata wa miaka 26 kutoka bila kikombe
1995-1999: VIKOMBE VITATU 
Miaka michache iliyofuata timu ilibadilika na Ferg alitengeneza vijana wenye vipaji vya aina yake kama  Gary Neville, David Beckham, Paul Scholes na  Nicky Butt ambao waliungana na  Giggs . hapo ulikuwa lazima uchanganyikiwe kwani katikati mwa kikosi hicho palikuwa na
  Roy Keane na  Scholes ilibidi ukubali upekee wa sehemu ya kiungo wa wachezaji hawa  kwani walitengeneza timu ya aina yake lakini timu hiyo ilikuwa na wachezaji wawili mapacha hatari zadi ambao unaweza kufikili kuwa walikuwa wamezaliwa siku moja au pamoja lakini sio kweli kwani mmoja ni raia wa uingereza na mwingine anatoka visiwa vya kule caribean tunawazungumzia   , Andy Cole na  Dwight Yorke ambao walitengeneza seshemu kali zaidi ya ushambuliaji  .
Teddy Sheringham na  Ole Gunnar Solskjaer na kijana kutoka  Tobago   walidhihirisha , bila shaka , siku ambayo waliushangaza ulimwengu baada ya kufunga mabao mawili na kuimaliza  Bayern Munich na kushinda ligi ya mabingwa ulaya mwaka  1999 .
Kwa wakati huo  Schmeichel alichaguliwa na kujulikana kuwa ndiye mlinda mlango bora zaidi ulimwenguni .hakika hata nje ya kiwanja kwa maana ya benchi la akiba kulikuwa na vijana kama  Jaap Stam,kijana hatari zaidi ambaye alikuwa tayari . hakuwa peke yake  Ronny Johnsen, Henning Berg  au Wes Brown wakiwa pamoja , Mholanzi huyo , hakika ulikuwa huwezi kushinda makombe kama haukuwa na kikosi kama hicho .
2006-09 Mwaka wa mafanikio tena ulaya 
Baada ya miaka miinne bila ubingwa wa Ligi ya uingereza alitengeneza kikosi kingine ambacho kilikuwa na wachezaji bora zaidi lakini hawakulingana sana na wale wa mwanzo na alikuja na mfumo wa  4-4-2.
,alinunua wachezaji kadhaa ambao waliweza kukabiliana na mfumo wake pamoja na Cristiano Ronaldo, aliweza kushabihiana na  Wayne Rooney na aliongezeka kijana mwingine mwenye nguvu  Carlos Tévez ambao walifanya kazi kubwa zaidi kiwanjani .kikosi hiki kiliweza kutwa ubingwa wa ulaya katika fainali iliyochezwa kule
 Moscow dhidi ya Chelsea. Baada ya Schmeichel,walipita walinda milango wengi lakini  Edwin van der Sar alipokuja mholanzi huyu ailipata raha golini kwani alikuwa akisaidiwa na ukuta bora  ambao ulikuwa ukiongozwa na  Rio Ferdinand na  Nemanja Vidic , Ferguson aliendelea kujikusanyia nishani katika soka . mzee alikuwa akijivunia kundi la watu shupavu . Giggs, Nani na Ji-Sung Park ambaye alisaidiwa na  Dimitar Berbatov ambaye alisajiriwa kuongeza radha tofauti katika nafasi ya ushambuliaji
2012-13 Kizazi kipya 
Ferguson anakielezea kikosi chake cha sasa kuwa kina uwezo wakufanya mambo makubwa zaidi siku za usoni kikiwa na wachezaji wadogo zaidi kama akina  David De Gea, Phil Jones, Chris Smalling, Rafael, Danny Welbeck na  Tom Cleverley – wakiwa chini ya miaka  24 wakiwa na mengi ya kujifunza .
Lakini anaweza kuwa chagua. Jones na Smalling, Bila shaka  ,Wanauwezo wa kupigana na kuuonyesha ulimwengu kuwa watakuwa mabeki bora katika safu ya ulinzi ya katika miaka ijayo .
Kutoka na Umri wa  Ferdinand’ na majeruhi yasiyokwisha na bila kusahau matatizo kama hayo yanamkabili pia Vidic, muda wao wa kuwepo klabuni hapo unawaka kwa taa ya nyekundu . Kwa sasa, Jones anastahili  nafasi katika kikosi manchester united bado ina hazina kubwa sana ya kujivunia hasa katika soka kwani huwezi kuacha kusema kutakuwaje msimu ujao pale wachezaji kama Zaha, Van persie ,Shinji kagawa na wengine ambao unawafahamu watakapo ungana na David Moyes je kitashuka au kitapanda 
.
Na mwisho ...Hiki ndio kikosi bora kwetu  
 Fergie XI

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers