29 May 2013

TAIFA STARS YAPEWA DOZI YA FANSIDA NA POULSEN ADDIS ABABA


 

Kwa mujibu wa kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na vipindi vinne vya mazoezi kabla ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan (Nile Crocodile). Mechi dhidi ya Sudan itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Addis.
Sudan ambayo pia imeweka kambi yake mjini Addis Ababa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza juzi dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala kwa mabao mabao 2-0.

Wachezaji wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa 'Barthez', Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Nadir Haroub 'Cannavaro', Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mcha, Amri Kiemba, Salum Abubakar 'Sure Boy', Simon Msuva, John Bocco, Vincent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd 'Chuji', Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda Marrakech alfajiri ya Juni 3 mwaka huu, ambapo itatua siku hiyo hiyo Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech

No comments:

Post a Comment