21 May 2013

WARWANDA WAINGIA KANDARASI YA MIAKA MIWILI NA Augsburg YA UJERUMANI

Rwanda Training 

Klabu ya soka ujerumani inayoshiriki ligi ya nchinini humo ya Bundesliga  Augsburg na kampuni ya kijerumani ya  afya ya meno  Mamisch imetangaza kuingia kandarasi ya miaka miwili na mabingwa wa Rwanda  Rayon Sports.

kwa mujibu wa mipango yao, Augsburg itakuwa ikitoa mipira mia moja kila mwaka, pea nne za jezi ,na vifaa vingine vinanvyo husiana na soka hasa kiufundi  ,wakati kampuni hiyo Mamisch ya afya ya meno itasaidia zaidi katika mwasala ya kifedha..
Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Rayon Sports , Abdallah Murenzi ameeleezea ushirikiano huo utaipatia ahueni timu yao hasa katika ndoa ambayo wamefunga na klabu hiyo hasa msimu ujao .

Kandarasi hiyo ya miaka miwili  kwa mujibu wa murenzi unaweza kuongezwa kutokana na maendeleo ya Timu hiyo msimu ujao .
“Tunaamini kuwa kandarasi hii itawanufaisha washirika wote wawili .

No comments:

Post a Comment