24 May 2013

Wolfsburg YA UJERUMANI YAVUNJA REKODI YA LYON KUTOFUNGWA MECHI 118

Wolfsburg


Klabu ya soka ya  Wolfsburg ya ujerumani imewafunga mabingwa mara mbili wa ligi ya mabingwa ulaya ya wanawake Lyon goli moja kwa bila 1-0 na kutwaa ubingwa wa ulaya .
Martina Muller's alipiga pernati katika kipindi cha pili na kuhitimisha ufalme wa LYON kutofungwa mechi ya  118 za mashinano bila kufungwa .
Ushindi huo wa uliopataikana katika uwanjawa wa  Chelsea' Stamford Bridge inamaana kuwa  Wolfsburg, ambao hawakushinda taji lolote miaka iliyopita, sasa wameshinda taji lao la tatu msimu huu .wameshinda ligi kuu ya ujerumani ya Bundesliga na kombe la ujerumani 
.
  Mchezaji bora wa  mechi hiyo Lena Goessling amesema : "kwa jinsi mambo yalivyotokea katika majuma mawili yaliyopita ni kama ndoto ."
Kocha wa Wolfsburg  Ralf Kellermann ameelezea ushindi huo kuwa ni kielelezo tosha cha kuwa wameonyesha ufundi wa hari ya juu na kuongeza kuwa anavipenda sana hivi viwanja vya uingereza.
  Aidha kocha wa Lyon  Patrice Lair amesema : "Tumeumia sana, japokuwa hatuja poteza mara kadhaa. hatukupoa sana kiwanjani na tunahitaji kuongeza juhudi kidogo ."

No comments:

Post a Comment