19 June 2013

FEDHA ZA IKIMBIZA TAIFA CUP HADI MWAKANI

Michuano ya Kombe la Taifa inayoshirikisha timu za mikoa ya Tanzania (Taifa Cup) haitafanyika tena mwaka huu kutokana na sababu za ukosefu wa fedha, imeelezwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kuwa wameshindwa kupata wadhamini wa michuano hiyo na hivyo haitafanyika.
 
Hata hivyo, Wambura aliongeza kuwa mashindano hayo yatafanyika mwakani baada ya kukamilika kwa mazungumzo yao na kampuni iliyojitokeza kuidhamini.
 
"Hatutakuwa na Taifa Cup mwaka huu kwa sababu hatuna fedha za kulipia gharama za usafiri na malazi ya timu shiriki. Mwakani tunaamini itafanyika kwa sababu tuko katika mazungumzo na kampuni ambayo imejitokeza kudhamini michuano hiyo," alisema Wambura bila kuitaja kampuni hiyo.
 
Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa mashindano hayo kutofanyika kutokana na kutopata wadhamini.
 

No comments:

Post a Comment