24 June 2013

GRAND MALT NA KAZI KUBWA YA KUINUA MICHEZO TANZANIA


 

Timu za Baraza la Wawakilishi za mchezo wa soka na netiboli, mwishoni mwa wiki zilikabidhiwa vifaa vya michezo vya aina mbalimbali ili kuziwezesha kushiriki mashindano mbalimbali kwa uwezo zaidi.
 
Vifaa hivyo vilitolewa na kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Zanzibar.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Idd, Meneja Masoko wa Grand Malt, Fimbo Butallah alisema, wataendelea kuwekeza katika michezo kwani wanaamini itatoa fursa kubwa kwa watu mbalimbali kushiriki na hata kujiongeza vipato vyao.

No comments:

Post a Comment