HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

5 June 2013

MAGARI YA TAIFA STARS YAKAMWA NA Flamingo Auction Mart KISA TFF YADAIWA 50 MILINI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvueaSvEoSDJTZ3BKLvTM1NWlZsr4OeT9mmEAJujd3D8cCWKqV4EmTzCtwO0DpG50eGeYXkJwVPBfig477O-IfL9DVKwbhCHuXzZLFAEo1s-zUfhoJfHc2FQwOHj3zJzyCAS0M5dG6jtE/s1600/gari+kuvutwa+(2).JPG 
 SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) leo wamejikuta wakipata aibu ya mwaka baada ya Kampuni ya
Flamingo Auction Mart, kuyapiga tanganyika jeki mabasi ya shirikisho hilo kutokana na deni la zaidi ya
Sh.50 milioni la Kampuni ya Safina Holding ya jijini Dar es Saalam.

Kampuni hiyo ya Flamingo leo ilitia timu kwenye ofisi za shirikisho hilo kufuatia amri ya Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kinondoni ikitaka zoezi la ukamataji magari hayo hadi Juni 30 liwe limeshakamilika.
Fedha hizo za Safina Holding zimetokana na hifadhi ya baadhi ya timu zilizoshiriki michuano ya Kombe
la Kagame mwaka jana na Yanga kuibuka kidedea.

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhoERRM2uMOE9X9mnESzm2GYaxFjyrSDHM4wFR_1uwdrV3RGK1HddTumXz7p_o1FyvI0zIkBLaLAN_5BUoa12SxnkZgmKSTGRixmF6VUAj_WQkJDmpAPXZ9q9w3iPbGW7ZRM-AbS27ZJg8/s1600/kuzuia+gari+zisitoke+(4).JPG 

Magari ambayo yameamriwa na mahakama hiyo kukamatwa ni basi aina ya Yutong lenye namba za usajili
T 581 CGR pamoja na Toyota Mini Bus lenye namba za usajili T 528 ASJ.

Lakini tofauti na amri hiyo ya Mahakama maofisa hao wa Flamingo walijikuta kwenye wakati mgumu
baada ya kuingia kwenye mzozo na maofisa wa TFF na kuzuka zogo kubwa huku maofisa hao wa TFF
wakiongozwa na Katibu mkuu Angetile Osiah kuzuia magari hayo yasichukuliwe.

Maofisa hao wa Flamingo wakiongozwa na Meneja Operation wao Noel Nyalila walitinga kwenye ofisi
hizo na kulifunga gari lenye namba za usajili T 528 ASJ aina ya Coster na kulivuta kwenye gari lao lenye
namba T 972 ABJ Jay Ambe, lakini walishindwa kuondoka nalo baada Osiah kuwaogoza wafanyakazi
wake kuzuia kwenye geti.

Wafanyakazi hao wa TFF waliamua kuzuia kwa kuegesha magari yao binafsi yenye namba T 643 BJW na
lingine lenye namba T 507 BER, hivyo kuzuia magari yaliyoamriwa kuchukuliwa.
Michuzi credit

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers